Hamorapa Kwishaaa! Meneja Wake Afunguka Mazito

Athuman Omary ‘Hamorapa’.

 

UBUYU wa leo unatakiwa uumun’gunye taratibu, ukipenda unaweza kushushia na maziwa maana unaambiwa mzee wa kiki ambaye alijizolea umaarufu miezi kadhaa iliyopita, Athuman Omary ‘Hamorapa’, kibarua chake tayari kimeota mbawa kwa meneja wake, Irene Sabuka. Irene Sabuka ndiye yule meneja wake aliyemsaidia kumtoa kisanii na zile mbwembwe zote, lakini sasa unaambiwa mambo ‘kwishnei’.

 

TUJIUNGE NA MLETA UBUYU WETU

Chanzo chetu makini ambacho ndicho mleta ubuyu wetu kilipepeta mambo kuwa, mwanamuziki huyo aliliamsha dude la meneja wake huyo baada ya kujitokeza kwa promota na kudai kuwa anaweza kumsaidia kupata shoo mbalimbali mikoani. Chanzo hicho ambacho ni mkereketwa na ubuyu wa mastaa kilizidi kutonya kuwa, baada ya promota huyo kuanza kumchukua Hamorapa na kufanya shoo mikoani, hakukuwa na mrejesho wowote wa fedha kwa meneja huyo badala yake walidai kuwa shoo hazikufanya vizuri.

IRENE ADAI KUTUMIA MIL. 70

“Yaani huyo promota na Hamorapa kila wanapokwenda mikoani, wakirudi hawana fedha wakati Irene alishatumia karibia shilingi milioni 70 kwa ajili ya kumtoa mwanamuziki huyo na kuwa juu kisanaa,” alisema sosi huyo.

 

MENEJA ATIBUKA ZAIDI

Mleta ubuyu huyo anasema kuwa, jambo hilo ndilo lililomtibua zaidi meneja huyo ni baada ya mwanamuziki huyo kuchukuliwa tena na promota huyo bila taarifa yoyote juu ya ni wapi walikokwenda. “Sasa kitu ambacho kilimfanya Irene akasirike zaidi ni kuwa promota huyo alimchukua Hamorapa, bila taarifa na kuondoka naye hivyo kumkasirikia na kumtaka amchukue moja kwa moja na asiwe tena chini yake,” kilifunguka chanzo hicho. HUYU

 

HAPA IRENE

Ijumaa Wikienda, kama kawaida yake, baada ya kupata ubuyu huo lilimtafuta Irene ambapo alipoulizwa kuhusu hilo

alisema kuwa, anachojua kuwa yeye alichukuliwa na promota huyo kwa kurubuniwa hivyo na yeye aliamua kunyanyua mikono ili aendelee naye. “Ninachojua huyo promota alijifanya anataka kumsaidia kumbe alishaona amepata jina, akataka kumrubuni na mimi nimeamua kumuacha tu kwa sababu ninajua ni wapi nilipomtoa,” alisema Irene.

 

HAMORAPA ASOMEWA MASHTAKA

Ijumaa Wikienda lilimtafuta Hamorapa na kumsomea mashtaka yake ambapo alidai kuwa, yeye anachojua bado Irene ni meneja wake na kama siyo ataliweka wazi baadaye. “Kuna vitu vimetokea kweli ila ninachojua Irene bado ni meneja wangu na ninamuomba Mungu tumalize tofauti zilizopo,” alisema Hamorapa.

 

NENO LA MHARIRI

Kama anavyosema Hamorapa ni jambo la kumuomba Mungu ili wamalize tofauti zao kwani wote wawili wametoana mbali

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Toa comment