The House of Favourite Newspapers

Hamtaamini Luis Miquissone Huyooo Anaenda Azam FC Simba Yatajwa

0
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Luis Miquissone raia wa Msumbiji.

AZAM FC imedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao, ni baada ya kukubali kutoa kitita cha dola 300,000 (zaidi ya Sh 710.5Mil) kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Luis Miquissone raia wa Msumbiji.

Mshambuliaji huyo aliyetolewa kwa mkopo klabu ya Abha inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia akitokea Al Ahly ya Misri hivi karibuni alitajwa kurejea Simba kwa ajili ya msimu ujao lakini ikaonekana fedha anayotaka alipwe ni nyingi.

Azam wanataka kukamilisha dili hilo la Luis, ikiwa ni saa chache baada ya kumsajili Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutoka.

Mmoja wa mabosi wa Azam FC, ameliambia Championi Ijumaa kuwa asilimia hamsini mazungumzo yamekamilika kati ya kiungo huyo na uongozi wa timu hiyo.

Bosi huyo alisema kuwa hivi sasa wanakamilisha mazungumzo ya mwisho na kiungo huyo kwa kukamilisha dili hilo ambalo atachukua mshahara wa Dola 20,000 (Sh47.3Mil) kwa mwezi.

Aliongeza kuwa muda wowote dili hilo litakamilika na kiungo huyo atajiunga na Azam ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tunakaribia kuipata saini ya Luis, hivi sasa tupo katika mazungumzo ya mwisho kukamilisha dili hilo la usajili kutoka klabu yake iliyomtoa kwa mkopo Al Ahly.

“Wametupa ofa ya dola 300,000 kama kweli tunamuhitaji mchezaji huyo, ambayo yote hiyo itakwenda kwa mchezaji ni baada ya timu yake kutaka kumtoa kwa mkopo.

“Alitakiwa ajiunge na Simba kwa mkopo, lakini imeshindikana ni baada ya kushindwa kutoa dau hilo la usajili ambalo ni dola 300,000, hivyo kama mambo yakienda sawa, basi tutampa hiyo pesa,” alisema bosi huyo.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ hivi karibuni alizungumzia hilo la usajili kwa kusema kuwa: “Tayari tumemalizana na wachezaji watatu kati ya hao yupo mmoja mzawa, na tutawatambulisha mara baada ya kukamilika kila kitu.”

Kwa upande wake, Meneja Mwasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema wamepeleka maombi kwa Klabu ya Al Ahly ili kumsajili tena Luis ili msimu ujao akiwashe Msimbazi.

“Tupo tayari kumnunua mchezaji kutoka popote pale kama wahusika wakikubali maombi yetu bila shaka tutakuwa naye msimu ujao.

“Miquissone ni mchezaji mzuri sana na ana uwezo wa kurejea na kutupa kitu kikubwa Simba, ila kwa sasa hatuwezi kusema sana kwa kuwa bado ana mkataba na Al Ahly hivyo wakiwa tayari kutuuzia tena muda wowote ataonekana kwetu,” alisema Ahmed.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

ALLY KAMWE AFUNGUKA DAU LA FEI TOTO KWENDA AZAM – “AKAENDELEZE MASHUTI YAKE”

Leave A Reply