The House of Favourite Newspapers

Hans apewa masharti Azam Fc

 

UONGOZI wa Azam FC, umempa masharti kocha wake mpya, Hans van Der Pluijm kuwatumia wachezaji vijana katika kikosi chake cha kwanza kama ilivyo falasafa ya timu hiyo kuwaendeleza vijana.

Hans ametokea Singida United huku akiwa amewahi kuifundisha Yanga tangu 2013 (aliondoka kwa muda mwaka 2014) hadi 2017.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema kuwa, moja ya makubaliano waliyoafikiana na kocha Hans ili kufanya kazi hapo ni kuhakikisha anawapa kipaumbele wachezaji vijana jambo ambalo wamekubaliana.

“Tumekubaliana na Hans aweze kuwatumia wachezaji vijana kwa kuwa falasafa yake ni kutowatumia vijana, hivyo amekubaliana na uongozi na atawapa nafasi.

“Hivyo wadau watarajie mchanganyiko wa wachezaji wakubwa na vijana katika kikosi cha Azam msimu ujao kama ilivyo kawaida kwa kuwa tumekubaliana na kocha, hivyo kila kitu kitakwenda sawa,” alisema Jaffar.

Azam imekuwa ikizalisha wachezaji wengi vijana katika kikosi chao ambapo wamekuwa wakiwapandisha kila msimu ili kuweza kuwapa uzoefu.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.