The House of Favourite Newspapers

Hans Pope Amekamatwa na TAKUKURU

MWENYEKITI wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope,  amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea nchini Marekani.

Hans Pope alikamatwa juzi na kujumuishwa kwenye kesi ya utakatishaji fedha na kughushi nyaraka inayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange, maarufu kwa jina la Kaburu, ambao walikamatwa mwaka jana.

 

Septemba 15, mwaka huu, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, alitangaza kuwa yeyote atakayewapata mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na mwenzake Frank Lauwo atapata zawadi nono.

 

Hans Poppe na Lauwo walikuwa wakitafutwa ili waunganishwe kwenye kesi hiyo ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

Comments are closed.