The House of Favourite Newspapers

Hans Poppe Apandishwa Mahakamani Kisutu Dar

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe,  leo amefikishwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu kesi inayomkabili ya madai ya kutoa taarifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi, kifungu 106(1) A& C (i) cha Income Tax Act sura ya 332 R.F 2008, kati ya Machi 10, 2016 na Septemba 30, 2016.

Poppe na mfanyabiashara, Franklin Lauwom  wamefikishwa  katika mahakama hiyo, saa tatu na nusu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani.

 

Aprili 30, 2018, mahakama hiyo iliamuru washtakiwa Hans Poppe na Lauwo wakamatwe popote walipo.

 

Mahakama hiyo ilitoa amri hiyo baada ya upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai,  kuieleza kuwa wamewatafuta washtakiwa hao tangu Machi 16 mwaka huu bila mafanikio

 

Poppe alikamatwa juzi  na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaamwakati akirejea nchini ambapo  ameunganishwa kwenye kesi inayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva,  na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Comments are closed.