The House of Favourite Newspapers

Hans Poppe: Namuonea Huruma Kaburu

0
Zacharia Hans Poppe

NA SWEETBERT LUKONGE | CHAMPIONI |GPL

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutomfikiria vibaya makamu wa rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kwa kumuona kama yeye ndiye tatizo ndani ya klabu hiyo.

Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akishangilia na wanachama wa Simba.

Poppe aliyasema hayo juzi baada ya kuibuka kwa uzushi kuwa Kaburu ni miongoni mwa watu ambao waliosababisha yeye atangaze kujiuzulu nafasi yake hiyo ndani ya Simba kabla ya kutangaza tena kutengua uamuzi wake huo. Jumapili iliyopita, Poppe alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake ndani ya Simba kutokana na kile alichodai ni uongozi wa juu wa klabu hiyo kwenda kinyume na makubaliano ambayo walikuwa wamekubaliana na Mohammed Dewji ‘MO’ na kuingia mkataba na Kampuni ya SportPesa, bila ya kumshirikisha.

Akizungumza na Championi Jumatano, Poppe alisema maneno hayo ambayo yamekuwa yakizungumzwa dhidi ya kiongozi huyo siyo ya kweli na anamuonea huruma sana. “Siyo kweli kuwa kaburu ndiye aliyesababisha mimi nitangaze kujiuzulu, haya maneno nimekuwa nikiyaona watu wanazungumza zungumza tu. “Unajua huyu ndugu yangu namuonea huruma sana, kila kitu kikitokea utaambiwa ni yeye, hakuna mtu mwingine anayehusishwa zaidi yake kitu ambacho siyo kweli,” alisema Poppe.

Leave A Reply