The House of Favourite Newspapers

Hapa Mr Blue Kule Zanzibar Stars, Dar Live

0

Na Mwandishi wetu| RISASI JUMAMOSI | Mikito Nusunusu

HII ikufikie kwa wewe mpenda burudani kuwa Sikukuu ya Idd kutakuwa hakutoshi baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Mr Blue kupagawisha sambamba na kundi kongwe la Taarab nchini, Zanzibar Stars ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alianza kwa kulisifia Kundi la Zanzibar Stars ambalo limekuja katika sura nyingine baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

“Zanzibar imerudi upya ikiwa na vichwa vikali kama Sabaha Muchacho, Zubeda Mlamali, Ally Jay, Mosi Suleimani, Jokha Kassim na wengine weeengi hivyo mashabiki wa Muziki wa Mwambao wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia wakifanya yao kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live.

“Pia ukiachana na Zanzibar Stars usiku huo tutakuwa na Mr Blue anayebamba na vibao vingi ikiwemo Baki Na Mimi, kundi la Makhirikhiri kutoka Tanzania, Wakali Dancers na wengine wengi kwa kiingilio kiduchu cha shilingi 5,000,” alisema Mbizo.

Leave A Reply