The House of Favourite Newspapers

Happines Sanga Mwanafunzi Bora wa Chuo Kikuu Ardhi

0
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akimpa cheti mwanafunzi bora wa mwaka huu wa masomo Happiness SangaX

 

WANAFUNZI 96 wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wametunukiwa tuzo mbalimbali kutokana na kufanya vizuri kitaaluma kwa mwaka wa masomo 2021/22.

Wanafunzi hao wamekabidhiwa tuzo hizo leo  Desemba 2, 2022 chuoni hapo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Evaristo Liwa, kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi hao. Mwanafunzi wa kike aliyeibuka mshindi wa jumla ni Happiness Sanga.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akimpa cheti mmoja wa wanafunzi wanaohitimu Jumanne

 

Akizungumza kwenye hafla hayo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. John Lupala amesema sherehe za kuwazawadia wanafunzi hao kila mwaka zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali.

 

Aliwapongeza wadau hao na kuwaomba waendelee kuunga mkono jitihada za wanafunzi hao kwani zawadi mbalimbali zinazotolewa na wadau hao zimekuwa zikisaidia kuongeza ari ya utendaji kazi kwa wanafunzi.

 

Prof. Lupala alisema tuzo hizo zimekuwa zikisaidia sana kuongeza tija kwenye maisha ya wanafunzi ya kielimu na kiuchumi huko wanakokwenda kufanyakazi.

Mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Happines Sanga

 

“Kwenye sherehe za mwaka huu tuna wanafunzi 96, kati yao wasichana ni 50 na wavulana ni 46 ambao wamefuzu kupata tuzo na zawadi mbalimbali kwa vipengele mbalimbali vya kitaaluma,” alisema Profesa Lupala.

 

Aliwapongeza wanafunzi wote waliopokea tuzo hizo na kuwataka waendelee kuweka jitihada kwenye masomo yao ili waje kuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wenzao na jamii kwa ujumla.

 

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Liwa alisema sherehe za utoaji tuzo Chuoni hapo zitafuatiwa na shughuli ya Mahafali siku ya Jumanne tarehe 6 Desemba ambapo wahitimu 930 wa ARU wa Shahada mbalimbali watatunukiwa Stashahada zao na aliwapongeza kwa kufikia hatua hiyo muhimu kwenye maisha yao.

 

“Nawapongeza sana wahitimu na baadhi yao wamekuwa wakipokea tuzo mbalimbali kwa miaka kadhaa mfululizo hii inamaanisha kwamba kwenye juhudi ya kweli mafanikio hupatiana ni matumaini ya chuo kuwa juhudi hizo mtaziendeleza kwenye shughuli za ujenzi wa taifa,” alisema

Aliwataja baadhi ya wadau waliotoa tuzo hizo kuwa ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bodi ya Wathamini Tanzania (VRB), Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Ukadiriaji Ujenzi (AQRB), African Property Limited, Taasisi ya Wabunifu na Wakadiriaji Ujenzi (TIQS), Mekon na Webb Uronu and Partners.

Leave A Reply