Mke Asimulia Alivyomuua Mumewe Kwa Bahati Mbaya Wakiwa Kwenye Ugomvi, Asota Jela Part 1&2 #HardTalk Video
MWANADADA Raheli Nyange, amesimulia mkasa uliomtokea wa kufungwa gerezani kwa miaka minne kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa mumewe na aliyoyapitia.
Kupitia Kipindi cha The Hard Talk kinachoendeshwa na mtangazaji @lillianmwasha_ , mwanadada huo ameeleza kuwa mumewe alikuwa na kawaida ya kumpiga kila anapokunywa pombe na kwamba siku hiyo kulitokea ugomvi kati yao, akamsukuma mumewe ambaye kwa bahati mbaya alijigonga kichwa na kupoteza maisha.