Harmo Afunguka Kofia ya JPM
STAA wa muziki na bosi wa lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize,’ amefunguka kupewa heshima ya kofia na RaisJohn Magufuli, kwenye kampeni wilayani Chato, Geita.
Harmo amesema kuwa ni heshima kubwa kwake na amefurahi kutokana na jinsi rais alivyomheshimu.
Kupitia meneja wake, Beauty Mmari ‘Mjerumani’, amesema kuwa ni heshima kwao na ni kitu kizuri.
‘Ni kitu kizuri tunashukuru kwa mwendelezo wa mheshimiwa rais kutambua mchango wa kazi za vijana na kuwakubali katika kazi zao…Rais akifanya chochote juu yako ni heshima kubwa,” alisema.
Story: Jackline Wandiba (TUDARCo)




