The House of Favourite Newspapers

Harmo asakwa kwa deni la mamilioni

0

DAR: Mambo si mambo kwa mkali wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’, inadaiwa kuwa kuna jamaa wanamsaka kwa deni la mamilioni ya fedha huko Mombasa nchini Kenya, IJUMAA linakupa mchapo kamili.

ALIKWENDA KUFANYA SHOO

Vyanzo vya habari kutoka nchini Kenya, vililieleza Gazeti la IJUMAA kuwa, Harmo alikwaa msala huo hivi karibuni alipokuwa amekwenda kufanya shoo.

“Shoo iliandaliwa na mtangazaji wa Milele FM, anaitwa Jalango ambaye pia ni staa mkubwa wa komedi hapa Kenya. Sasa walikubaliana kwamba atalipwa shilingi milioni 1 ya Kenya (zaidi ya shilingi milioni 22), lakini mbwembwe zake Harmo ndiyo zikamponza,” kilieleza chanzo chetu kutoka nchini humo.

ALIOMBA RANGE ROVER LA KUTANULIA…

Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, Harmo alipofika Mombasa, aliwaomba waandaaji wampatie gari aina ya Range Rover Sport ili atanulie na kufanya road show (matangazo ya barabarani).

“Waandaaji walimkatalia kwa kumuambia siyo huduma ya lazima na kwamba mashabiki wanaweza kufanya fujo na kuharibu gari, lakini Harmo akasema kama wakiharibu yeye atagharamia. Wakawa hawana jinsi, wakamtafutia hilo gari aina ya Range Rover linalomilikiwa na jamaa ambaye ni komedian mkubwa tu hapa Kenya anaitwa Jalango,” kilisema chanzo hicho.

MISELE MITAANI

Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, baada ya kupewa gari hilo ndipo akaanza kuzunguka mitaani na kugawa fedha, lakini alipofika kwenye Mtaa wa Mama Ngina (Mombasa) akawa anawarushia mashabiki pesa.

“Hapo ndipo kukaibuka vurugu na kukanyagana, kwani mashabiki walimvamia, wakavunja kioo cha side mirror.

“Walipomweleza kuwa atagharamia kama alivyoahidi awali, alikubali kulipa. Sasa walipokuwa wanataka kumlipa pesa yake kabla ya shoo, walimueleza kuwa watamkata shilingi laki 2 za Kenya (zaidi ya shilingi milioni 4 za Kibongo) akakataa.

“Shoo yake ilikuwa alipwe shilingi milioni moja (ya Kenya) sasa alipoambiwa atakatwa hiyo laki mbili na kwamba atapewa laki nane, aligoma,” kilisema chanzo.

AJITETEA

Chanzo hicho kilieleza kuwa, Harmo alijitetea kuwa hawezi kukatwa fedha hizo wakati naye ameshamwaga pesa nyingi kwa mashabiki, lakini jamaa wakamwambia basi hawamlipi na asubirie ‘kuipata freshi’.

HARMO AKASEPA

“Harmo akasepa zake bila kufanya shoo, akarudi zake Bongo kuendelea na mishemishe zake maana aliona jamaa hawako serious, akawaachia mpunga wa shoo, akachimba,” kilisema chanzo hicho.

WAMKOMALIA POLISI

Chanzo hicho kilidai kuwa, baada ya jamaa kuondoka bila kufanya shoo hiyo pamoja na kulipia gharama za kioo, walimfungulia mashtaka Polisi, hivyo anatafutwa ili alipe gharama hizo.

“Yaani jamaa wamekomaa, wanataka alipe zile gharama za kioo, lakini pia anatakiwa alipe gharama za hasara waliyoipata kwa kutotokea kwenye shoo ambazo hawajaziweka hadharani ni shilingi ngapi,” kilisema chanzo.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Harmo, lakini hakupatikana hewani kwa maelezo kwamba yupo nje ya nchi.

MENEJA ANENA

Alipotafutwa mmoja wa mameneja wa Harmo, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ kuhusu ishu hiyo alisema walishamalizana nayo na kwamba ni vitu vya kawaida kwa wasanii.

“Hiyo ishu tulishai-clear (kuimaliza). Hayo ni mambo ya kawaida kwa wasanii kuwa na mbwembwe kwa mashabiki wao, lakini tulishalimaliza,” alisema Mjerumani.

TUJIKUMBUSHE

Hii si mara ya kwanza kwa Harmo kukwaa msala nchini Kenya, Machi mwaka jana alipata msala wa Serikali baada ya kuzuia wimbo wake yeye na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Kwangwaru kutopigwa nchini humo kwa kukiuka maadili.

Leave A Reply