The House of Favourite Newspapers
gunners X

Harmo Atikisa Ndinga za Mamilioni

0

MAFANIKIO ya mtu yanapimwa kwa vigezo mbalimbali ikiwemo mali anazozimiliki na jinsi anavyoishi.  Wasanii wengi Bongo wamekuwa na majina makubwa, lakini ukiangalia mali walizonazo ni za kawaida au hazifanani na ukubwa wa majina yao.

Lakini kwa staa wa Bongo Fleva; Rajab Abdul ‘Harmonize’, mambo ni tofauti kwani akiwa na miaka minne tu kwenye muziki, tayari anatikisa na ndinga za mamilioni. Uchunguzi wa Gazeti la Risasi Jumamosi umebaini kwamba, Harmonize au Harmo ameshamiri na anamiliki magari mbalimbali.

Ilibainika kwamba, miongoni mwa magari anayomiliki ni Toyota Alphard ya mwaka 2018 lenye thamani ya Dola za Kimarekani 10,378 (zaidi ya shilingi milioni 23.8 za Kitanzania). Ukiachana na Toyota Alphard, ilibainika kwamba, Harmo pia anamiliki gari aina ya Audi TT RS Roadster (open roof) ambalo mara nyingi hulitumia kwenye misele yake akiwa mwenyewe. Hili lina thamani ya Dola za Kimarekani 28,535 (zaidi ya shilingi milioni 65 za Kibongo).

Gari la tatu analomiliki Harmo ambalo huwa analitumia kwenye misafara yake mara nyingi kama ile ya shoo na akiwa amepata mwaliko sehemu kwa ajili ya sherehe au mikutano ni Land Cruiser V8, toleo la mwaka 2016 lenye thamani ya Dola za Kimarekani 41,082 (zaidi ya shilingi milioni 94 za Kitanzania).

Ilibainika pia, mbali na gari hizo tatu, pia jamaa huyo anamiliki gari ambalo hutumika kusambaza chakula cha bure kwa mashabiki wake ambalo amelipa jina la Konde Boy Mgahawa. Gari hilo ni aina ya Mitsubishi Fuso lenye thamani ya Dola za Kimarekani 25,549 (zaidi ya shilingi milioni 58 za Kibongo). Kwa ujumla, uchunguzi huo ulibaini kwamba, Harmo anamiliki magari au ndiga za thamani ya shilingi milioni 240 za Kitanzania.

STORI: AMMAR MASIMBA, RISASI

Leave A Reply