The House of Favourite Newspapers
gunners X

Harmo kuiteka Dar

0

RAJABU Abdul ‘Harmonize’ au Harmo ana jambo lake Dar, taarifa zinasema kwamba siku hiyo mkali huyo wa Bongo Fleva, ataliteka jiji zima la Dar na watu wote watakuwa pale Mlimani City kumshuhudia.  Meneja wa Harmonize, Beauty Mmary ‘Mjerumani’ amesema Februari 14, mwaka huu itakuwa ni siku ya historia Bongo kwani mkali huyo anakwenda kuzindua albamu yake inayokwenda kwa jina la Afro East.

“Itakuwa ni siku ya tofauti sana. Ni uzinduzi ambao haujawahi kutokea Bongo, hivyo niwaombe mashabiki wa muziki wetu watufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii na wale watakaopata bahati ya kualikwa, basi tutashuhudia pamoja uzinduzi huo,” alisema Mjerumani.

Kwa upande wake Harmo, amesema anatamani watu wote wangekuwepo kwenye shoo hiyo ya uzinduzi, lakini itashindikana. Hivyo wale watakaopata nafasi, watapata kitu cha tofauti na kuahidi kugawa mialiko yake.

“Binafsi ningetamani sana kila anayesoma hii apate nafasi ya kuja pale Mlimani City hiyo tarehe 14/3/2020 ili kujionea hili balaa linaloenda kutokea kwa sababu, ila kwa kuwa ipo nje ya uwezo wangu, basi hao watu 500 watakaopata nafasi ya kupewa mialiko, watakuwa pale kwa niaba ya wotee!

“Team @kondegang nikuibie siri tu…@ mjerumani_255 x @ jembenijembe x @choppa_ tz washapanga majina ya watu wao wataowaalika, ila mie nina card zangu (18) kwa ajili ya wanangu ambao mngetamani kuwepo pale siku hiyo, unachotakiwa kufanya follow @afroeast2020 kwenye Instagram kisha wewe niandikie jina la ngoma unayohisi itakuwa ni kali kuliko zote, unajichukulia kadi zako,” alisema Harmo.

Stori: Neema Adrian, Risasi

Leave A Reply