#GlobalCelebrityUpdates: Harmo Rappa Apigwa Chupa Maisha Basement Kisa ‘Kiboko Ya Mabisho’ – (Pichaz& Video)

 

Good morning mdau, leo kwenye Celebrity Updates ninazo zile zilizobamba over the weekend ikiwemo hii ya msanii anaechipukia kwa kasi sana Bongo Flevani Harmo Rappa kupigwa chupa akiwa stejini Maisha Club. Ilikuwaje? Acha nikutonye…

Usiku wa jumapili 02 April 2017, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diana Nyange alikuwa na show yake ya ‘USIKU WA KOMELA’ iliyokusanya mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki Maisha Basement kushuhudia burudani iliyoandaliwa na mwanadada huyo na miongoni mwa wasanii waliyopanda stejini kuperfrom usiku huo ni pamoja na msanii anayeongoza kwa matukio mengi mitandaoni Harmo Rappa.

Akiwa stejini anaperform wimbo wake mpya ‘Kiboko ya mabisho’, Harmo Rappa alijikuta akirushiwa chupa iliyokuwa na bia na moja ya mashabiki waliohudhuria show hiyo kisa mstari mfupi unaosikika kwenye wimbo wake; tulikuwa WASAFI kabla ya WCB, maneno yao machafu hayaniharibii CV…. Bila kujua wala kutegemea shabiki huyo (ambaye inanokeana wazi ni Team WCB for life) alimrushia Harmo Rappa chupa ya bia lakini alifanikiwa kuikwepa chupa hiyo na hivyo kunusurika kuumia.

Kitendo hicho kiliamsha fujo ndani ya Maisha Basement, mabaunsa walifanikiwa kumtoa Harmo Rappa stejini na kumsaka kijana aliyesababisha fujo hizo lakini mpaka wanafanikiwa kumtia mikononi mwao jamaa huyo alikuwa ameshachakazwa na wananchi wenye hasira kali.

Alivyohojiwa na kuulizwa kwa nini amefanya hivyo au pengine ametumwa na watu wa upande wa WCB, kaka huyo alikana na kusema kuwa hakutumwa na mtu yoyote ila ni vile hampendi tu Harmo Rappa na anashangaa yeye ni nani mpaka ajifananishe na WCB. Baada ya hapo kijana huyo alichukuliwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Mabatini, Kijitonyama na kufungiliwa mashitaka. 

Meneja wa Harmo Rappa amesema msanii wake anaedelea vizuri ila bado ana mshituko.

Hizi ni baadhi ya picha alizofanikiwa kuzinasa ripota wetu wa Global Publishers:

Vipande Vipande vya chupa vulivyomkosa Harmo Rappa.

Kaka aliyemrushia Harmo Rapa chupa ndiyo huyu, na hivi ndivyo alivyokuwa baada ya kula kipigo na mashabiki.

Harmo Rapa akiwa kwenye mshituko baada ya kunusurika kupigwa chupa.

Baada ya kula kipigo Maish Basement, kaka huyo akafikishwa kwenye Kituo Cha Polisi

ITAZAME NA HII VIDEO HAPA CHINI:

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

PICHA/ VIDEO Na: Emelda (Global Publishers).

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.Tecno


Toa comment