Harmo Rappa Abamwa Akipiga Mzigo Usiku Mnene

Harmolapa wa kwanza (kulia) akiwa mzigoni hapo alimshtukia paparazi wetu

MWANAMUZIKI chipukizi ambaye hivi karibuni anatikisa kjwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutokana staili yake aliyokuja nayo ya kufananishwa na mwanamuziki wa kundi la W.C.B Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ jana amebambwa na kamera yetu usiku maeneo ya kariakoo akipakua vioo.

Hamorapa mwenye T-sheti nyeusi

 

Mwanamuziki huto alipoulizwa kuhusiana na kazi ile anayofanya alisema kuwa ile ni kazi yake nyingine ambayo amepewa kufanya na meneja wake aitwaye Irene Sabuka, kama moja ya kumfanya asilemae katika kazi moja tu  ya muziki.

“ Unajua bosi wangu hapendi nijibweteke na kazi moja tu hivyo ndio maana hata hapa napiga mzigo usiku huu baada ya kontena la vioo kufika  na ndio kazi yangu nyingine ninayojivunia” alisema Harmo.

Picha zote zikimuonyesha mwanamuziki akipiga kazi.

Imelda Mtema/GPL

 

 

 

 
Toa comment