The House of Favourite Newspapers

HARMONIZE; Acha ‘Drama’, Jifunze Kusimama Kiume

Har­monize

SIKU chache zilizopita, kilinuka kwenye mitandao ya kijamii, skendo kubwa ikiwa ni madai ya mwanadada mwenye asili ya Kizungu, Sarah ambaye yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa muziki wa kizazi kipya Har­monize, kudaiwa kumsaliti msanii huyo.

Ishu ilikuwa ni kwamba Sarah ameamua kumbwaga Harmonize na kuhamishia mapenzi yake kwa baunsa wa msanii Diamond Plat­numz, anayefahamika zaidi kama Mwarabu Fighter, kwa wafuatiliaji wa masuala ya burudani watakuwa wanam­fahamu vizuri ‘baunsa’ huyu kwa sababu kila Diamond al­ipo, naye anakuwa pembeni yake kumlinda.

Kwa ‘necha’ ya wasanii wa Wasafi, inawezekana kabisa kuwa suala hili likawa ni njia ya kutafutia ‘kiki’ kama am­bavyo wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda mrefu sasa, au inawezekana pia ikawa ni kweli lakini nisingependa sana kuzungumzia suala hilo, ukweli wanaujua wenyewe.

Ninachotaka kukizungum­za hapa, ni kwamba wakati ‘skendo’ hiyo ikiwa imepam­ba kwenye mitandao ya kijamii, mwanadada Wolper ambaye amewahi kuwa kwenye uhusiano na Harmo­nize, alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari kuhusu sakata hilo, akamsemea ‘mbovu’ Sarah.

Akadai eti ni ‘mlezi wa wana’ akimaanisha kwamba Mzungu huyo ana kawaida ya kuwahonga wanaume anapohitaji kuwatumia kimapenzi kisha baada ya hapo, akishatosheka ana­hamishia majeshi kwa mwanaume mwingine.

Kimsingi alichoki­fanya Wolper kilikuwa ni makosa, kwa sababu uk­weli ni kwamba yeye na Harmonize walishaach­ana na kila mmoja akaendelea na maisha yake. Sasa linapotokea suala kama hilo, halafu Wolper akatoa maoni yake na kumzungumzia vibaya mwanadada huyo ambaye ana­toka na Harmonize, kimsingi linakuwa ni jambo la ajabu. sikutegemea kumsikia Wolper ak­iendelea kumzun­

gumzia tena Harmonize wala mpenzi wake kwa sababu uku­rasa wao ulishafungwa. Kitendo cha kuendelea kumzungumzia, tena kwa ubaya kinaonesha kwamba bado Wolper naye haja­komaa kiakili, hasa linapokuja suala la mapenzi.

Baada ya sakata hilo la Wolper, Harmonize naye akaamua kulipuka na kumshambulia vikali Wolper, akihoji kwamba yeye na Sarah nani ni mlezi wa wana? Aka­posti kile alichokiita kikosi cha kwanza cha wanaume waliowahi kutoka na Wolper na hapo ndi­po hasa ninapotaka kuzungumza na Harmonize.

Katika orodha hiyo, Harmonize amewataja wa­naume kadhaa, ambao wengine hivi sasa wapo kwenye ndoa, wengine wapo kwenye uhusiano ‘serious’ na wengine wanaendelea na maisha yao mengine tofauti kabisa.

Miongoni mwa wa­liotajwa, yupo Chid Mapenzi ambaye kwa sasa ni mume halali wa msanii wa Bongo Muvi, Shamsa Ford. Yupo pia Jux ambaye naye yupo kwenye uhusiano siriasi na mwanadada Vanessa Mdee, achana na hao wengine ambao sijawataja. Sasa unajiuliza, wakati Harmo­nize anawataja wanaume hao, alikuwa hajui kwamba hapigani

na Wolper tu bali anawain­giza kwenye matatizo watu wengine ambao hata hawahusiki na ugomvi wao huo wa kitoto? Muda mfupi baada ya kuposti hicho alichokipoti, mwanadada Shamsa Ford alikuja juu na kumtolea mapovu Harmonize akimtaka amheshimu Chid Mapenzi kwani hivi sasa yeye ni mume wa mtu.

Yawezekana Shamsa ni nembo tu ya wengine wengi walioumizwa sana na alichoki­fanya Harmonize na akaamua kufunguka. Pengine wengine wanaendelea kuumia ndani kwa ndani, pengine wengine wame­jikuta kwenye ugomvi mkubwa na wapenzi wao kwa sababu tu ya utoto wa Harmonize.

Sikia Konde Boy, kuna wakati unatakiwa kujitambua kwamba wewe siyo mvulana tena, bali mwanaume na unatakiwa kusi­mama kiume. Kitendo ulichoki­fanya, cha kutaja orodha ya waliowahi kutoka na ‘ex’ wako, siyo tu kimeonesha jinsi ulivyo ‘chenga’, bali pia umeonesha kwamba bado haujakomaa.

Kibaya zaidi umesahau kwamba tayari unao mashabiki wanaokutazama kama kioo chao, lakini pia ukasahau hata hao uliowataja wanao mashabiki, wazazi, ndugu na ma­rafiki, utajisikiaje utakapogundua kwamba ulichokifanya kime­sababisha ndoa ya mtu fulani ikavunjika?

Ufike wakati sasa ujitambue na kuachana na ‘drama’ zisizo na kichwa wala miguu, hata kama Wolper alikosea, hiyo haikuwa njia sahihi ya wewe kukabiliana naye. Act like a man!

HASH POWER

Comments are closed.