HARMONIZE AFUNGUKA KUWATUKANA WAKENYA

Rajab Abdul ‘Harmonize’

MKALI wa Bongo Fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdul ‘Harmonize’ amefungukia tuhuma ya kutukana Wakenya kwa kuwaita maskini kwamba ni hali ya kutokuelewana tu, lakini hakumaanisha vibaya. 

 

Tukio hilo lililotokea mjini Mombasa, Kenya wakati akipafomu kwenye Wasafi Festival lililofanyika Desemba 31, mwaka jana na kuwaambia wanampenda kwa sababu Wakenya ni maskini wenzake ndiyo maana wanamuonesha mapenzi ya kweli katika muziki wake, lakini wao walitafsiri vibaya.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Harmonize alisema hata yeye hakutegemea kama wangemtafsiri tofauti.

“Unajua Kiswahili cha Wakenya na Watanzania ni tofauti ndiyo maana walitafsiri vile, ila mimi niliwaambia kwa nia nzuri tu kuwa watu wengi wananiuliza kwa nini Wakenya wanakusapoti sana kwenye muziki wako? Nikawaambia ni kwa sababu wao ni maskini kama mimi ghafla nashangaa watu wananishautia huku wanatikisa vichwa.

 

“Huku wakisema usituite maskini maana tumelipa viingilio, sikutegemea kama itafikia hivyo, lakini nilitamani wajue kuwa sikumaanisha vibaya nawezaje kuwaita maskini wakati wao ndiyo wananiwezesha jamani,” alisema Harmonize

Stori: Shamuma Awadhi

Loading...

Toa comment