The House of Favourite Newspapers

Harmonize Afunika Mlimani City (Picha +Video)

0
Harmonize na mpenzi wake Sara walivyowasili Ukumbi wa Mlimani City, Dar wakati kuzindua albamu yake ya Afro East usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2020.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Kahali maarufu Harmonize au Konde Boy usiku wa kuamkia leo alijaza umati mkubwa wa mashabiki ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar wakati akizindua albamu yake ya Afro East.

Katika shoo hiyo pamoja na kufurika wageni waalikwa zaidi ya 500 pia ilivamiwa na mashabiki zake wengine zaidi ya idadi hiyo na kupafanya eneo hilo litapike watu na kukosekana pakukanyaga.

Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi.

Kutokana na kufurika kwa umati eneo hilo nusu ya mashabiki waliofika eneo hilo waliishia nje kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa kadi mwaliko au waliotaka kutumia kadi moja kwa zaidi ya mtu mmoja.

Msanii Dora akihojiwa na mapaparazi
Mashabiki wa Harmonize waliishia hapa na kuambiwa waishie kuangalia hapahapa
Msanii wa Bongo Muvi, Duma akiingia ukumbini.

Leave A Reply