The House of Favourite Newspapers

Harmonize Aingilia Sakata Mtoto wa Ibraah, Ampa Ushauri Mzito

0

HARMONIZE au Konde Boy Mjeshi; ni staa wa muziki nchini Tanzania ambaye ameingilia kati sakata la msanii wake, Ibraah kudaiwa kuzaa na kufanana na mtoto ambaye mama yake anadai ni wa msanii huyo.

 

Harmonize amemshauri Ibraah kumkubali mtoto huyo huku akiahidi kusaidia katika malezi.

Harmonize amemwambia Ibraah; “Brother tuletee huyu mfalme tutakopa, tutaiba, tutatapeli ilimradi mkono uende kinywani. Mungu na masela haina kufeli!”

 

Bosi huyo wa Lebo ya Konde Gang ameendelea kumshauri Ibraah achukue hatua ya kufanya kipimo cha DNA (vinasaba) na mtoto huyo ili kutatua fumbo la kuhusika kwake na kujua kama kweli ni damu yake.

 

Harmonize ameonesha kukubaliana na maoni kuwa motto huyo anafanana na Ibraah na tayari amemkubali kuwa mjukuu wake.

 

“Nenda tu, ukajiridhishe na DNA upate amani ya moyo ila huyu Chinga. Mjukuu wa mzee Konde Boy,” amesema Harmonize.

 

Mtoto anayezungumziwa ametambulishwa mitandaoni kwa jina la Zein Ibrahim Nampunga na ni mwanawe mwanadada Clyna almaarufu Sugar.

 

Hivi karibuni Sugar alijitokeza kulalamika kuwa Ibraah ametelekeza jukumu la malezi ya mtoto huyo na kumwagiza awajibike.

Sugar alimtuhumu Ibraah kwa kuwa na ‘utoto’ mwingi huku akidai kuwa amekuwa akiogopa kuitwa baba.

 

“Labda ana utoto. Nimemzidi umri kwa mwaka mmoja. Nimezaliwa 1997 yeye amezaliwa 1998. Kitendo cha kuitwa baba amekuwa akikiogopa sana. Drama ni nyingi. Ibraah hamhudumii mtoto. Amekuwa mtu mgumu. Hata hivyo ananiheshimu sana,” alisema.

 

Sugar alisema kuwa yupo tayari kwa Ibraah kufanyia mtoto wake DNA ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye baba mzazi.

Katika kile kilichoonekana kuwa jibu lake kwa mwanadada huyo, Ibraah alisema; “Msinipe watoto wa watu mimi sina mtoto.”

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply