The House of Favourite Newspapers

HARMONIZE AMPIGA BAO DIAMOND

MAISHA yanakwenda spidi mno na kutangulia kwenye maisha haya siyo kufika!

Hicho ndicho kinachotokea kwa mastaa wawili wakubwa wa Bongo Fleva walio ndani ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ na bosi wake, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ juu ya suala zima la kuchumbia.

 

Pamoja na kumzidi kwa vingi, taarifa ikufikie kuwa Harmonize amempiga bao Diamond au Mondi juu ya ishu ya kuchumbia.

 

Wiki iliyopita, Harmonize alipiga magoti mbele ya mchumba’ke wa kitambo, Sarah Michelotti na wazungu kibao huko jijini Roma nchini Italia akiwa Mwafrika pekee kwenye shughuli hiyo na kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo.

 

HARMONIZE AMPIGA BAO MONDI

Harmonize amempiga bao hilo Mondi ambaye mbali na kushindwa kumuoa mrembo Tanasha Donna Oketch kama alivyoahidi Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day), hata pete ya uchumba ameshindwa kumvisha.

 

UCHUMBA WA HARMONIZE NA SARAH

Harmonize alifanikiwa kutimiza azma yake ya kumvisha Sarah pete hiyo ya uchumba katika tukio hilo ambalo lilifanyika ukweni kwake, Roma nchini Italia na kuhudhuriwa na ndugu wa upande mmoja tu wa mwanamke hivyo kuibua maswali kama yote.

Gazeti la Amani linafahamu kwamba kabla ya tukio hilo, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye sintofahamu.

Katika sintofahamu hiyo, Harmonize alidaiwa kuchepuka na mrembo ambaye picha zao zilikuwa ‘zikitrendi’ kwenye mitandao ya kijamii.

 

PICHA ZA PETE

Hata hivyo, wakati ishu hiyo ikiwa ya moto ndipo Harmonize na Sarah walipoonekana kumaliza tofauti zao kwani siku chache baadaye zilivuja picha zao zikimuonesha jamaa huyo akimvisha Sarah pete ya uchumba.

Tukio la Harmonize kumvisha Sarah pete ya uchumba lilihudhuriwa na watu wachache ambao walionekana ni watu wa karibu wa Sarah.

 

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, Harmonize aliposti video ikimuonesha akimvalisha pete Sarah na kuisindikiza na maneno yaliyosomeka:

”If you think she said no!” Akimaanisha; “Kama ulidhani atasema hapana!”

 

PONGEZI KAMA ZOTE

Watu mbalimbali wakiwemo viongozi kupitia ukurasa huo wa Instagram walimpa Harmonize pongezi kama zote kwa hatua hiyo kubwa ya kujitambulisha ukweni na kumvalisha pete ya uchumba msichana wake huyo ambaye hivi karibuni amekuwa video queen katika wimbo mpya wa jamaa huyo unaofanya vizuri unaokwenda kwa jina la Niteke.

 

Mwanamuziki ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ni mmoja wa viongozi waliotoa pongezi kwa Harmonize. Aliandika; ”Congratulations young bro na Mungu awalinde.”

 

Hata hivyo, Diamond hakusema chochote wala kutoa pongezi kwa kutumia mitandao ya kijamii kufuatia jambo hilo la kheri alilolianzisha Harmonize.

Pamoja na zoezi hilo, lakini Harmonize hakuweka wazi suala zima la harusi yao inatarajiwa kufungwa lini.

HARMONIZE AFUNGUKA

Akifungukia tukio hilo, Harmonize alisema kuwa, baada ya tukio hilo kubwa kifuatacho ni ndoa bila kujali kwamba wao ni dini tofauti kwani yeye ni Muislam wakati Sarah ni Mkristo.

“Lakini naamini tutafunga ndoa ya Kiislam kwa sababu mimi ni mtoto wa Kiislam, mama na baba yangu ni Waislam, lakini Sarah baba yake (Michelotti) ni Mkristo, bahati mbaya alishafariki dunia, lakini mama yake ni Muislam.

 

“Kwa hiyo kuna asilimia kama 98 ya ndoa kuwa ya Kiislam japokuwa tunaamini Mungu ni mmoja tu, kwa huyo ninaisubiri hiyo siku kubwa kwenye maisha yangu.”

 

ILIKUWA SAPRAIZ?

“Kuhusu kumvisha Sarah pete, mimi na mama ndiyo tulikuwa tunawasiliana, kwa hiyo tuliwapigia ndugu na marafiki zake tukawapa taarifa, lakini Sarah mwenyewe alikuwa hajui chochote kwa hiyo alikuwa na furaha sana ndiyo maana akawa analia.

 

“Sikwenda na mtu yeyote wa upande wangu kwa sababu niliamua kufanya hivyo ili kumuonesha ni kwa jinsi gani ninampenda kwa ajili ya maisha yetu wawili na siyo mtu mwingine.

“Kuhusu mahari ya Sarah hatukuzungumza chochote kwani ukiona mahari ujue ndoa ipo karibu, kwa hiyo ilikuwa ni kuchumbia kwanza halafu mambo ya mahari yatakuja baadaye.

“Unajua wenzetu mahari siyo pesa au ni shilingi ngapi. Kikubwa wanachoangalia unampenda vipi mtoto wao.”

 

TULIKOTOKA

Kabla ya kuwa na Sarah, Harmonize alikuwa kwenye mapenzi motomoto na staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe kisha wakamwagana.

Stori: Sifael Paul, Amani

Comments are closed.