The House of Favourite Newspapers

Harmonize Ataja Sababu Kumsaini Ibra

0

STAA wa muziki wa Bongo Fleva kunako lebo ya Konde Gang, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ametaja sababu za kumsaini msanii mpya anayejulikana kwa jina la Ibra Tz katika lebo yake.

 

Harmonize alisema kuwa, uandishi na aina yake ya kuimba, ndiyo sababu kubwa ya kumsaini msanii huyo katika lebo yake.

 

“Ibra ni msanii ambaye anastaili yake ya kuimba, ubora katika uandishi, pia anatokea familia ya chini kama mimi. Hivyo, hawezi kuchezea nafasi ambayo ameipata,’’ alisema Harmonize, staa wa ngoma ya Bedroom.

Leave A Reply