The House of Favourite Newspapers

Harmonize Atangaza Fursa kwa Watangazaji na Ma Dj’s – (VIDEO)

 

Msanii Harmonize toka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ametangaza fursa ya kuwafanyia (utambulisho) jingles watangazaji na ma dj’s wa redioni. Amefunguka hayo kwenye akaunti yake ya instagram huku zikiambatana na shukrani kwa mashabiki pamoja na salamu za mwaka mpya.

 

“HERI YA MWAKA MPYA….!!! NDUGU ZANGU …!!! NINGEPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WAANDISHI WA HABARI PAMOJA NA MEDIA ZOTE AMBAZO ZIMEKUWA SAMBAMBA NAMI BILA KUWASAHAU DJ’S WOTE DUNIANI KWA KUUNGANA NAMI NA KUNI SUPPORT KUSOPPORT MUZIKI WANGU AMA KWA HAKIKA BILA NYINYI BASI PASINGEKUWA NA HARMONIZE HATA MUZIKI WENYEWE HUWENDA USINGEKUWEPO MWAKA 2018 UMEKUWA MWAKA WENYE KUONYESHA MWANGA AMA NURU YA MUZIKI KWANGU NAAMINI MAZURI MENGI YAPO MBELE NINGEOMBA MUENDELEE NA MOYO HUWO HUWO WA UPENDO NA IMANI KUNIVUMILIA NINAPOKOSEA KWANI MIMI SIJAKAMILIKA HASA UKICHANGANYA NA UJANA…!!!! LAKINI PIA NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA SHABIKI ZANGU AMBAO MUPO BEGA KWA BEGA NAMI KUHAKIKISHA TUNALIKAMILISHA KILA TULIPANGALO KWA UWEZO WA MUNGU….!!!!! HAKIKA NYINYI NDIO HARMONIZE MWENYEWE….!!!” Aliandika Harmonize

 

Baada ya kumaliza na kutoa shukrani kwa mashabiki na aliendelea kwa kutangaza fursa kwa wamiliki wa vituo vya redio, watangazaji na ma dj’s, “LAMWISHO NIOMBE KUWASILISHA HILI DOGO KWA WAMILIKI WA MEDIA WATANGAZAJI PAMOJA NA DJ’S WOTE….!!! KAMA UNGEPENDA MIMI NIKUPIGIE JINGLE AU TANGAZO LA REDIO YAKO BASI UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUCHUKUA NUMBER HI..! 👉 +255658135762 KISHA TUMA MAELEKEZO YAKO MFANO MIMI NI DJ FULANI KIPINDI FULANI YANI TUMA MAELEKEZO YAKO YOTE KUPITIA WHTSP NADHANI WATU WA MEDIA WASHANIELEWA NINACHO MAANISHA KISHA MWISHO WEKA EMAIL YAKO NAMI NITARECORD NA NITAKUTUMI KATIKA EMAIL YAKO HI NI KWA MEDIA WATANGAZAJI DJ’S WOTE DUNIANI……!!! LET’S GO…….!!!!!!!!!!”

 

TAZAMA VIDEO AKIFUNGUKA HAPO CHINI

@harmonize_tz atangaza fursa kwa watangazaji na Ma DJ’s, atoa namba za simu. #kondeboy #wcb

7 Likes, 0 Comments – Global Publishers (@globalpublishers) on Instagram: “@harmonize_tz atangaza fursa kwa watangazaji na Ma DJ’s, atoa namba za simu. #kondeboy #wcb”

 

Harmonize mpaka wakati huu anafanya vizuri na wimbo wake wa Paranawe akiwa na Rayvanny.

Comments are closed.