HARMONIZE AWEKA REKODI KWA WAZAZI

 STAA grade one wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ ameweka rekodi kwa kuwanunulia wazazi wake magari mapya na kuwafunika mastaa wote Bongo hivyo kuibua gumzo kama lote. 

 

Harmonize alifanya ishu hiyo kubwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar baada ya ‘kuwasapraizi’ wazazi wake hao kwa kuwazawadia magari hayo aina ya Toyota Harrier.

 

Harmonize anayeitumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) amekuwa akinukuliwa mara kwa mara kuwa alipitia msoto katika maisha magumu na wazazi wake hivyo kama amefanikiwa na wao lazima wawe na maisha mazuri.

Kwenye zoezi hilo, Harmonize magari hayo mawili aina ya Toyota Harrier ambapo moja ni la rangi ya silver na lingine ni la rangi nyeupe. Katika kuchagua, mama yake alichagua rangi ya silver na baba akajisevia la rangi nyeupe huku wakilengwalengwa na machozi.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusu zawadi hiyo kwa wazazi wake, Harmonize alisema katika maisha yake na wazazi wake walipitia mambo mengi, lakini walivumilia wakiamini ipo siku Mungu atawapa hivyo ni jukumu lake kuhakikisha wazazi wake wanakuwa na furaha.

 

“Wanapofurahi wazazi wangu na mimi ninapata baraka, ninawapenda wazazi wangu na nitaendelea kuwapenda kwani wamenitoa mbali,” alisema Harmonize ambaye ana mpango wa kuwahamishia wazazi wake jijini Dar kutoka mkoani Mtwara.

Katika wimbo wake unaofanya vizuri wa Never Give Up (Usikate Tamaa), Harmonize anaeleza namna ambavyo matatizo yalikuwa ni sehemu ya maisha yake na kwamba wazazi wake walikuwa naye bega kwa bega. Kufuatia tukio hilo la kuwapa wazazi wake magari hayo, baadhi ya mastaa walimpongeza huku wengine wakishauriwa kufuata nyayo zake.

 

Mastaa hao walimpa hongera huku wengine wakipata funzo la kuwakumbuka na kuwasaidia wazazi wao pindi wanapopata mafanikio yoyote. Ukiacha zawadi hiyo kwa wazazi wake, wiki kadhaa zilizopita, Harmonize alimpa zawadi ya gari rafiki yake wa tangu utotoni, Jose Wamipango.

 

Harmonize alimpa Jose gari jipya aina ya Toyota Swift kwa ajili ya kumpongeza katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Harmonize alisema Jose amekuwa rafiki yake tangu kitambo hata kabla ya kupata umaarufu na fedha.

“Hata kuiandika (Ngoma ya Never Give Up) niliandika nikiwa katika mazingira magumu sana nikiwa ghetto. “Nilikuwa ninaishi kwa mwanangu anaitwa Jose Wamipango. Nilikuwa naishi ABC, lakini mwanagu anaitwa Jose alikuwa anaishi maeneo ya Ilala (Dar) na familia yao kidogo ilikuwa iko freshi.

 

“So nilikuwa natoka zangu kuangalia studio tofautitofauti, nilikuwa nikichelewa naenda pale kwa mwanangu Jose, jamaa ana imani sana na mimi ndiyo maana nikaona zawadi inayomfaa ni gari,” alisema Harmonize.


Loading...

Toa comment