testiingg
The House of Favourite Newspapers

Harmonize, Briana Watanua na Ndinga la Sarah

0

DESEMBA mwaka jana, aliyekuwa mke wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul almaarufu Harmonize, Sarah
Michelotti alimtaka jamaa huyo
amrudishie gari lake aina ya Audi alilompa enzi za penzi lao shatashata.


Sarah alikwenda mbali zaidi na
kueleza kwamba, gari hilo ni lake na kwamba ndiye aliyelinunua, lakini Harmonize au Konde Boy Mjeshi hakuonesha kutikiswa na jambo hilo.


Hata hivyo, habari mpya ni
kwamba, kwa sasa jamaa huyo na mpenzi wake mpya aitwaye Briana wanatanua na gari hilo, jambo linaloibua minong’ono kwa mashosti wa Sarah wakimtaka akalichukue gari lake.

 


Katika kuthibitisha hilo, Gazeti
la IJUMAA lilifika nyumbani kwa Harmonize maeneo ya Mbezi- Beach jijini Dar na kuthibitishiwa kwamba jamaa huyo alikuwa ametoka na mpenzi wake huyo kwenda kwenye misele yao wakilitumia gari hilo lenye rangi ya kijani.


Ikumbukwe kuwa Harmonize na
Sarah walifunga ndoa September 2019 zikiwa ni siku chache tu baada ya msanii huyo kujitoa kwenye lebo ya Wasafi, walifunga ndoa baada ya kuwa kwenye mapenzi kwa zaidi ya miaka miwili.


Hata hivyo, mwaka 2020; mwaka
mmoja baada ya kubadilishana kwa viapo, ilitangazwa kuwa wenzi hao walikuwa wametengana kwa sababu ya tofauti zisizoweza kusuluhishwa ikiwemo kutuhumiana kuwa na uhusiano wa watu wa nje huku meseji zikinaswa walivyokuwa wanabadilishana taarifa na michepuko.

STORI; WAANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply