The House of Favourite Newspapers
gunners X

Harmonize na Kajala Waonekana Pamoja Kwenye Boti, Mashabiki Wapagawa – Video

0

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, ameonekana tena akiwa karibu na mpenzi wake Kajala, katika hafla maalum iliyofanyika ndani ya boti, hatua iliyozidi kuashiria kurejea kwa mahusiano yao.

Katika tukio hilo la faragha, wawili hao walialika marafiki wachache wa karibu, ambapo walionekana wakifurahi, wakicheka na kubadilishana maneno ya kirafiki, jambo lililovutia hisia za mashabiki waliotazama kupitia video na picha zilizokuwa zikisambaa mtandaoni.

Mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na muonekano huo mpya wa upendo na maelewano, wakiamini kuwa safari yao mpya ya mahusiano huenda ikawa yenye utulivu na ukomavu zaidi kuliko awali.

Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na wawili hao kuhusu mipango yao ya mbele, zaidi ya kuonekana wakifurahia muda wao pamoja.

Leave A Reply