The House of Favourite Newspapers

Harmonize: Nikifa Mungu Mlinde Kajala Namba Moja, Mama na Baba Konde, Namba Nne

0

Harmonize au Konde Boy; ni staa wa kimataifa wa muziki kutoka nchini Tanzania ambaye wikiendi iliyopita aliangusha bonge la shoo huko Goma ambako ni Mashariki mwa Kongo na kuacha historia ya aina yake.

 

Hata hivyo, kubwa ni baada ya Harmonize kuzuiliwa njiani kutokana na wingi wa mashabiki ambapo amesema kuwa ilibidi atumie boti kuondoka eneo la tukio kwa sababu watu na bodaboda walikuwa wamefunga barabara.

 

Katika maombi yake akiwa kwenye boti kuwakwepa mashabiki wake hao, Harmo amemuomba Mungu kama litatokea lolote baya katika maisha yake, basi mtu wa kwanza kumlinda ni mpenzi wake, Kajala kisha mama yake, baba yake na mwanawe huku akisema hana shaka na mashabiki kwani watapata burudani kutoka kwa Ibraah, Anjella na wengine walio chini ya lebo yake ya Konde Gang.

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa Konde Gang, Harmonize.

 

Harmonize amesema; “Mungu najua unajua kwamba nimemaliza kutesti sauti, sasa narudi hotelini, lakini bodaboda wameziba njia kwa hiyo tumeamua kuchukua boti ili tuwahi.

 

“Likitokea la kutokea lolote, basi Mungu nakuomba umline mke wangu Kajala Masanja namba moja, namba mbili na namba tatu ni Mama Konde na Baba Konde, namba nne ni Zuu Konde.

 

“Kuhusu mashabiki, siha shaka kwa sababu kuna vichwa na majembe kina Ibraah, Anjella, Killy na Cheed hivyo sina shaka.

Leave A Reply