The House of Favourite Newspapers
gunners X

Harmonize: Nimebezwa Sana

0

Harmonize au Konde Boy Mjeshi amefunguka kuwa, pamoja na mafanikio aliyoyapata, lakini hawezi kusahau nyakati ngumu alizopitia ikiwemo kubezwa sana katika miaka miwili ambayo  ameianzisha lebo yake ya muziki ya Konde Gang Music baada ya kujitoa Wasafi.

Konde Boy anasema; “Kwanza nawashukuru Watanzania wote kwa kusapoti Lebo ya Konde Gang ilianza kama ndoto ya kijana kutoka mtaani, lengo lilikuwa ni kuanzisha team ya kunisimamia mimi kama mimi na ilivyokamilika nilipata fursa ya kusimamia vijana wengine na kusimamisha wasanii wakubwa.

“Nichukue nafasi hii kumshukuru kila mtu ambaye anatusapoti, wakati naanza nlibezwa sana na hakuna mtu ambaye alitegemea hii lebo itakuwa kubwa kwa Afrika Mashariki. Kwa hiyo kikubwa tu ni watu tu waendelee kusapoti kuna makubwa yanakuja.”

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply