Harmonize: Rasmi Nimerudi kwa Wolper wangu!

PENZI ni kikohozi kulificha huwezi! Ndivyo ambavyo unaweza kusema kufuatia kinachoendelea kati ya mastaa wawili kutoka Bongo Flevani, Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.

 

Wawili hao wameendelea kuzua gumzo baada ya Harmonize kutangaza kurudi kwa Wolper wake ambaye alimwagana naye miezi kadhaa iliyopita.

Ishu nzima ilijiri usiku wa kuamkia juzi Jumamosi katika shoo ya Wasafi Festival iliyofanyika mjini Iringa na kusababisha mji huo kutikisika.

Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda kwenye Uwanja wa Samora, Harmonize alimpandisha stejini Wolper kama ‘sapraizi’ na kumwangukia akimuomba warudiane, jambo ambalo Wolper alilikubali mbele ya maelfu ya mashabiki wao.

“Naomba niseme wazi hapa hadharani kuwa nimerudi kwa Wolper wangu,” alisikika Harmonize.

Wiki iliyopita wawili hao waliozua gumzo mkoani Mtwara katika shoo ya kwanza ya Wasafi Festival baada ya kugandana mbele ya watu kwa dakika kadhaa wakioneshana mahaba kama yote.

 

Kufuatia kile kilichojiri mjini Mtwara ambapo Wolper alieleza nia yake ya kumrudisha Harmonize kwenye himaya yake ambapo wengi waliamini kuwa wawili hao wamerudiana maana wahenga walisema kiporo hakihitaji kupashwa na moto mwingi.

 

Kumbuka kabla ya sarakasi hizo mpya ilifahamika kuwa wawili hao walikuwa kwenye bifu zito hadi kufikia hatua ya kutupiana maneno machafu mitandaoni ambapo Harmonize alimpata mzungu aitwaye Sarah anayesemekana kuwa kwa sasa ni mjamzito.

 

Katika tukio la Iringa, wakiwa nyuma ya jukwaa kulikuwa na mawasiliano ya chini kwa chini kati yao ambayo yalikuwa ya siri kwa sababu walikuwa wamekaa sehemu tofauti huku wakipeana ishara.

Ijumaa Wikienda lilikuwa makini kuwafuatilia wawili hao hadi mwisho wa mchezo huo ili kujua kama kweli kuna kitu kinaendelea kati yao.

Wakati Harmonize anakaribia kupanda stejini, kuna jamaa alitumwa kwenda kumnong’oneza kitu Wolper.

Baada ya hapo, Harmonize aliondoka kuelekea stejini ambapo aliimba nyimbo mbili kisha Wolper alisaidiwa kunyanyuka na kuelekea upande ambao ulikuwa unamuwezesha kupanda stejini.

Hapo ndipo Harmonize alipoamuru taa zizimwe stejini kwani alikuwa na sapraizi kwa watu wake wa Iringa.

 

Wakati taa zikiwa zimezimwa, ulipigwa Wimbo wa Nambie ambao video queen alikuwa Wolper ndipo mwanadada huyo akapanda stejini na kuanza kucheza na Harmonize huku wakikumbatiana kimahaba kabla ya jamaa huyo kutangaza kumrudia rasmi Wolper.

 

Baada ya kushuka stejini watu wengi walitaka kufanya mahojiano na Wolper, lakini hakurudi nyuma ya jukwaa kwani alichukuliwa na wapambe wa Harmonize na kwenda naye moja kwa moja hadi kwenye gari na kuondoka.

HARMONIZE AGOMA KUMPANDISHA WOLPER JUKWAANI – VIDEO

Toa comment