The House of Favourite Newspapers

Harmorapa Kujifunza Kingereza kwa Mr. English

0
Harmorapa kujifunza Kingereza
Harmorapa.

BWA’MDOGO asiyekaukiwa matukio, Harmorapa anatarajia kuanza kujinoa katika suala zima la Lugha ya Kingereza kwa mtaalam wa kufundisha lugha hiyo, James Mramba ‘Mr. English’.

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kuona kuna fursa anaikosa katika suala zima la kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali hususan atakapokwenda kupiga shoo nje ya nchi.

Mr. English.

“Nimeamua kujifunza Kingereza na sehemu sahihi kwangu ni kwa Mr. English kwa sababu anatoa huduma za mobile.

Atanifuata nyumbani, najifunza private,” alisema Harmorapa. Mr. English anatoa huduma hiyo katika ofisi yake iliyopo Sinza-Mapambano na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0713 369805 au 0767 369805 ili aweze kukuhudumia popote ulipo.

STORI: RISASI VIBES

 

Tambwe na Chirwa Waenguliwa Kikosini Yanga

Leave A Reply