Harry Kane Atangazwa Kuachana na Tottenham na Kujiunga na Bayern Munich
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Uingereza na mfungaji kinara wa wakati wote wa Klabu ya Tottenham Hostpurs ‘Spurs’, Harry Kane ametangazwa kujiunga rasmi na klabu kubwa duniani kutoka nchini Ujerumani, Bayern Munich.
Kane amejiunga na Bayern kwa dau la pauni milioni 95 ambapo anatarajiwa kuanza kuonekana rasmi akiwa na jezi ya timu hiyo leo Jumamosi katika mchezo wa German Super Cup kati ya Bayern na RB Leipzig.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ameachana na Spurs akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa wakati wote wa timu hiyo, akitupia kambani mabao 280 katika michezo 435 aliyoitumikia klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, Premier League.
Kane alikuwa akihusishwa kwenda kwenye timu kubwa za Uingereza ikiwemo Manchester City na Manchester United huku pia akitajwa kutaka kujiunga na Real Madrid lakini ni Bayern ndiyo waliofanikiwa kupata saini yake.