The House of Favourite Newspapers

Harusi za Gharama Kubwa, Sherehe Mahotelini Vyapigwa Marufuku

somaliaweddingSOMALIA: Mji wa Bula Hawa nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashawishi vijana wengi zaidi kuoa.

Kamishna wa Mji wa Bula Hawa uliyo karibu na mpaka wa Kenya, Mohamud Hayd Osman amesema kwamba, mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.

Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 (sawa na TZS 350,000/=) pekee ambapo uamuzi huo umekuja baada ya maafisa kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.

Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.

“Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini,” alisema Osman.

Hatua ya kupunguza matumizi kuhusu sherehe za kifahari pamoja na matumizi mengine baada ya ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo. Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.

Wiki Moja Baada ya Ndoa, Masele Chapombe Amtongoza Upya Mke Wake

Comments are closed.