Kartra

Hassan Nassoro: Ninapiga Mashuti 30 Kila Siku

HASSAN Nasorro, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Polisi Tanzania amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ya kupiga mipira huru mara 30 kwa siku.

 

Nyota huyo ambaye ni chaguo la kwanza la Malale Hamsini ndani ya Polisi Tanzania ana uwezo mkubwa wa kuchezea mpira anavyotaka pamoja na kutoa pasi za uhakika kwa wachezaji wenzake.

 

 

Mbali na kuwa ndani ya Polisi Tanzania, Nassoro amewahi kutumika ndani ya kikosi cha Ndanda FC ambacho kinashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

 

 

Nassoro amesma kuwa amekuwa akifanya mazoezi muda mwingi lengo ikiwa ni kuweza kuwa bora. “Nipo vizui na ninapenda namna ambavyo tunashirikiana kwenye kazi yetu ya kusaka ushindi uwanjani.

 

 

“Kuhusu mipira iliyokufa nimekuwa nikifanya mazoezi ya kufanya hivyo kila siku ambapo ninapiga jumla ya mipira 30 nikiwa katikati ya uwanja. Jambo hilo kwangu ni kazi na ninafanya kwa kupenda hivyo sioni mashaka yoyote,” amesema.

 

 

Polisi Tanzania kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 9 na ina pointi 30 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.


Toa comment