The House of Favourite Newspapers

HATARI: Gari la Petroli Lalipuka Moto, Watu 10 Wapoteza Maisha – Video

Mlipuko mkubwa wa Moto umetokea katika Daraja Maarufu la Oteldola jijini Lagos nchini Nigeria jana Alhamisi, majira ya saa 1:30 jioni baada ya gari ya mafuta ya petroli kulipuka katika eneo hilo.

 

Inadaiwa mpaka sasa watu 10 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa huku magari zaidi ya 54 yakiwemo mabasi matano yamewaka moto huku taarifa zikieleza kuwa chanzo cha moto huo ni kutokana na kugoma kwa breki za lori hilo la mafuta.

Kulipuka kwa magari ya mafuta nchini Nigeria yamekuwa ni m,atukio ya kujirudia kila mara ambapo inadaiwa baada ya breki kugoma, lori hilo lilipoteza mwelekeo ndipo tank la mafuta likaanguka na kushika moto uliosambaa hata kwenye magari yaliyokuwa karibu nalo.

 

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ametoa pole kwa wote waliogushwa na tukio hilo wakiwemo wafiwa huku Msemaji wa Serikali ya nchi hiyo, Kehinde Bamigbetan akisema kuwa wanaweka mkakati wa magari ya mafuta kuanza kuendeshwa na madereva wenye uzoefu zaidi.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO

Comments are closed.