The House of Favourite Newspapers

Hatari yYa Kuishi Ili Mradi Siku Zinakwenda!

0

WIKI hii nataka kuzungumzia suala zima la kusaka mafanikio huku nikikuuliza wewe msomaji wangu kwamba, umeamua kufanikiwa katika maisha yako kwa kufanya nini hasa?

Wakati nasoma sekondari nilitamani sana kufanya kazi ya ndishi licha ya kwamba pia niliamini biashara inaweza kunifanya nikafi ka pale ambapo nilitamani kuwepo katika maisha yangu.

Kutokana na utashi wangu huo nilijikuta nikiamua kuchagua kuwa mwandishi na wakati huohuo mfanyabiashara huku nikiamini  wamba kazi hizi zitanipatia mafanikio.

Mafanikio ni mafanikio licha ya kwamba viwango vya kufanikiwa vinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mantiki hiyo basi naweza kusema nimefanikiwa kwa kiasi fulani licha ya kwamba nahitaji mafanikio makubwa zaidi.

Labda nikuulize wewe msomaji, ukiulizwa umeamua kuwa nani na kufanya nini katika maisha yako utajibu nini? Naamini kwa swali hilo kila mtu atakuwa na jibu lake.

Usishangae kumsikia mtu akisema ameamua kuwa kahaba na mwingine akakueleza kwamba ameamua kuwa mwizi katika maisha yake.

Lakini pia unaweza kumsikia mtu akisema, ameamua kuwa daktari ama mfanyabiashara katika maisha yake. Kimsingi kila mtu ana chaguo lake.

Unachotakiwa kujiuliza ni kwamba, je kwa kuwa mwizi au kahaba unaweza kuwa na mafanikio ya kudumu katika maisha yako? Hilo ndilo swali la msingi.

Wakati mwingine inakuwa ni afadhali na mtu aliyeamua kufanya kazi ya kubeba mizigo ama kuzibua mtaro katika maisha yake kuliko Yule ambaye hajaamua afanye nini katika maisha yake ili kujiletea maendeleo. Hawa ni wale wanaoishi kibubusa bubusa ili mradi tu siku zinakwenda.

Ninavyoona ni kwamba, karne hii si ya kuishi kibubusa na kushukuru Mungu kwa kuiona siku nyingine bali unatakiwa kujiuliza baada ya Mungu kukujalia kuiona siku hiyo nyingine, utaitumia vipi?

Kitu cha msingi ni kujiwekea mikakati madhubuti ya vipi utaendesha maisha yako katika kila siku ya Mungu.

Imefi ka wakati sasa wa kuamua ufanye nini na uwe nani katika maisha yako la sivyo utabaki kuwa si chochote wala si lolote na mwishowe Mungu ataona hana sababu ya kukubakiza ulimwenguni wakati huna chochote unachokifanya.

Katika maisha ukijaribu kuchunguza kwa makini utakuta kwamba wengi wa waliofanikiwa ni wale waliochagua mafanikio.

Waliamua kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanafika pale ambapo walitaka kufi ka.

Hii inathibitisha kwamba katika maisha kila kitu ni uamuzi na ndiyo maana nadiriki kusema wale ambao wana nguvu za kutosha na       afya njema lakini ni maskini, naamini wameamua kuwa maskini katika maisha yao. Watu hao wakiamua kuwa matajiri pia wanaweza.

Kwa kumalizia niseme tu kwamba hakuna hata mmoja wetu ambaye ameletwa hapa ulimwenguni ili awe si lolote wala si chochote. Kila mtu ana nafasi yake ambayo akiitumia vizuri ana uwezo wa kuwa na maisha bora.

Leave A Reply