The House of Favourite Newspapers

Hathari za mjamzito kuwa na tatizo la moyo

TATIZO la kufunguka mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa cha moyo na kuzuia kupita kwa damu ya kutosha kwenda kwenye mshipa mkubwa wa damu (aorta) ambao huhusika kuzungusha damu ndani ya mwili hujulikana kitaalamu mitral stenosis na ni hatari kwa mama na mtoto aliyetumboni.  Tatizo hili la kufunguka mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa husababishwa na homa inayojulikana kama rheumatic fever, mtu anaweza kuzaliwa na hali hii.

Tatizo hilo pia husababishwa na matibabu ya saratani za kifua kwa kutumia tiba ya mionzi na mkusanyiko wa madini aina calcium kwenye milango hiyo ya moyo. Kati ya hizo sababu hapo juu, inayosababisha kutokea kwa tatizo hili kwa wakubwa ni homa ya rheumatic fever, ambayo hufuatia maambukizi ya vimelea vya bakteria aina ya streptococci kwenye koo au ngozi ambayo haikutibiwa kikamilifu.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kutopata dalili au viashiria vyovyote vile mpaka pale atakapotimiza umri wa miaka 20 hadi 50. Hata hivyo wengine wanaweza kupata dalili na viashiria vya tatizo hili wakati wa kufanya mazoezi au kazi yoyote ambayo inaongeza mapigo ya moyo, msongo mawazo na wakati wa kubeba ujauzito.

DALILI ZAKE

Dalili na viashiria vyake ni; mjamzito kushindwa kupumua vizuri wakati wa kujishughulisha na shughuli yoyote ile na wakati mwingine kutopumua vizuri hata muda wa kupumzika kama tatizo limekuwa kubwa sana. Dalili nyingine ni kukohoa makohozi yaliochanganyika na damu kidogo, kushindwa kupumua ukiwa umelala bila mto au kitanda kunyanyuliwa.

Dalili nyingine ni kushtuka usiku na kubanwa pumzi, kubanwa na pumzi wakati wa mazoezi, uchovu, kusikia au kuhisi mapigo yako ya moyo na kuvimba miguu yaani lower limb edema. Tatizo hili la ujauzito kuambatana na kufunguka kwa mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa limegawanyika katika hatua tatu:

Mosi; hatua kali kiasi, pili; wastani na tatu; kali zaidi. Dalili na viashiria vya tatizo hili huwa mbaya zaidi pale mjamzito anapokuwa na tatizo la kufunguka kwa mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa katika hatua ya wastani na kali zaidi, maana ujauzito pekee uhitaji kuongezeka kwa ujazo wa damu hasa miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito na upungufu unaotokana na milango ya moyo kushindwa kufunguka hufanya hatua ya kujifungua ya mjamzito kuwa ya hatari sana.

HATARI KWA MTOTO ALIYE TUMBONI

Hivyo; ujauzito ulioambatana na tatizo hili husababisha moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, kupiga bila mpangilio wake na kuwa hatari kwa mtoto kuzaliwa kabla ya wakati yaani premature delivery, au mtoto kuzaliwa na uzito mdogo au mtoto kufa kwenye mfuko wa kizazi au baada ya kuzaliwa.

Vifuatavyo ni vipimo muhimu vya kupimwa mjamzito. Echocardiogram- Kipimo hiki huonyesha tatizo hili vizuri hadi hatua gani lilipofikia, ukubwa wa vyumba vya moyo na uwezo moyo kufanya kazi, na iwapo moyo kama haufanyi kazi yake vizuri. ECG- Huonyesha kiwango cha mapigo ya moyo na vilevile kama moyo unapiga bila mpangilio. Vipimo hivi vyote ni salama kwa mjamzito.

MATIBABU NA USHAURI

Ni muhimu kwa mgonjwa kuonana na daktari pamoja na kuandikiwa dawa ambazo hutumika kudhibiti dalili na viashiria vya tatizo hili, dawa hizo ni za aina ya furosemide, spironalactone na digoxin.

Kwa wajawazito walio kwenye hatua ya wastani na kali zaidi ya tatizo hili watahitaji tiba ya kuzibua mlango huo unaotenganisha vyumba vya kushoto vya moyo, kwa kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja mpaka kwenye moyo na kuweza kuzibua mlango huo. Baada ya tiba hii wanaweza kujifungua kwa njia ya kawaida mtoto mwenye afya.

Baadhi ya wajawazito watahitaji kufanyiwa upasuaji wa kuzalisha mtoto na hapo baadaye kurudi hospitali kurekebishwa au kubadili huo mlango wa moyo wenye tatizo la kutofunguka

Comments are closed.