The House of Favourite Newspapers

Hatima ya Unaibu Rais wa Rigathi Gachagua Madarakani Kujulikana leo

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua

MUSWADA wa kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua madarakani utawasilishwa Bungeni leo, Oktoba 1, 2024, Saa 8:30 Mchana. Ikiwa Muswada huo utapitishwa, Spika wa Bunge, Moses Wetangula atawasilisha uamuzi huo kwa Spika wa Seneti Amason Kingi kwa hatua zaidi

Gachagua anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Rais William Ruto, huku akikabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi, kufadhili fujo za Gen Z katika Maandamano, kutoa siri za Serikali na Kuchochea Ukabila

Kiongozi wa Wengi na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah alithibitisha kuwa hoja dhidi ya Gachagua itawasilishwa mbele ya Bunge saa nane unusu leo kwa saa za Afrika mashariki.

Uwasilishaji wa hoja hiyo utahitaji kuungwa mkono na wabunge 233 na kuna taarifa zinazodai kuwa wajumbe 302 tayari wametia saini.

Wanaomshitaki Gachagua wanadai kuwa amekiuka Kifungu cha 10 cha katiba, wakisema matamshi yake hadharani yamekuwa ya uchochezi na yanaweza kuibua chuki za kikabila.

Pia anatuhumiwa kukiuka vifungu vya 147, 148,174,186 na 189 vinavyozungumzia mwenendo na wajibu wake kama msaidizi mkuu wa Rais.

Pia atajitetea dhidi ya madai ya kujipatia mali kwa ufisadi na kutumia pesa za walipa kodi kwa njia isiyo halali. Mali hiyo inasemekana kusambazwa katika kaunti za Nyeri, Nairobi na Kilifi.

Gachagua ametoa onyo kwa Rais Ruto, akisema kwamba kama Washirika wake wataendelea na hoja ya kumwondoa, Ruto anaweza kupoteza uungwaji mkono wa eneo la Mlima Kenya. Amehimiza uongozi wa Ruto kutulia na kuruhusu Serikali kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.

KAULI ya SEMAJI LA UBAYA UBWELA BAADA ya KUTUA DAR – ”SISI TUNAANGALIA ALAMA 3”…

Leave A Reply