ALIKIBA AKUBALI OMBI LA DIAMOND, ATAWASAPOTI WCB
IKIWA ni siku mbili baada ya staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ambaye piani Mkurugenzi wa Wasafi Media, kutangaza kuwa angetamani kumuona msanii mwenzake, Alikiba, akiungana naye kwenye tamasha lake la Wasafi Festival, hatimaye Kiba amekubali ombi hilo na kuahidi kutoa sapoti.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba ameandika; “Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.
“Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi.
“Tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrinkili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa. Management #RockstarAfricayangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa.
Wasafi Festival inatarajiwa kuzinduliwa Novemba 24 mkoani Mtwara ambapo baadaye Iringa, Morogoro na mikoa mingine itafuata.
Comments are closed.