The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Bilionea Namba Moja Duniani, Elon Musk Aununua Mtandao Wa Kijamii wa Twitter Kwa Dola Bilioni 44

0
                                     Tajiri namba moja duniani, Elon Musk

Tajiri namba moja duniani, Elon Musk hatimaye amefanikisha dili lake la nguvu la kuununua mtandao wa kijamii wa Twitter kwa dau la dola za Kimarekani dola bilioni 44 pamoja na kununua kila hisa kwa dau la dola 54.20.

Kwa siku kadhaa, bosi ya menejimenti ya Mtandao wa Twitter ilikuwa kwenye majadiliano makali na bilionea huyo ambaye amedai kwamba lengo la kuununua mtandao huo ni kuhakikisha kwamba haki ya kila mmoja kutoa maoni yake inatekelezwa kikamilifu.

Baada ya majadiliano marefu, hatimaye uongozi wa Twitter umefikia muafaka wa kukubaliana na dau nono lililowekwa mezani na Elon na kufanya dili hilo kuwa miongoni mwa biashara kubwa zilizofanyika katika miezi ya hivi karibuni.

Ameahidi kwamba atahakikisha mtandao huo unakuwa na huduma bora zaidi kwa mtumiaji ili kurahisisha mawasiliano na uhuru wa kutoa maoni.

Leave A Reply