HATIMAYE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI LATINGA MTAANI – PICHAZ
TIMU nzima ya wafanyakazi wa Global Publishers, wakiongozwa na Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, mapema leo wametinga mtaani kulinadi gazeti la Spoti Xtra ambalo ni jipya na ambalo limekuwa likiingia mtaani siku za Jumaili na sasa limeanza kuingia mtaani kila siku ya Alhamisi kwa bei ya shilingi 500.
Akizungumzia ujio huo wa gazeti hilo la Spoti Xtra kila Alhamisi, Mrisho amesema lengo kubwa ni kumaliza kiu ya wapenzi wa habari za michezo na ndiyo sababu kubwa ya kuliingiza mtaani siku hiyo.
Wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra ambao walichangamka kulinunua maeneo ya Stendi ya Makumbusho na maeneo ya makutano ya mataa ya Morocco-Kinondoni, wamelipongeza kwa mwonekano mzuri na kwa namna ambavyo limesheheni habari za michezo.
“Kiukweli nyie watu wa Global mmetusaidia sana kuliingiza gazeti hilo siku ya Alhamisi kwani tumekuwa tukikosa habari za michezo na kubaki tukitafakari nini cha kufanya, hongereni sana,” alisema mmoja wa madereva wa stendi ya makumbusho aliyejitambulisha kwa jina la Masudi Khamis.
PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS
Comments are closed.