HATIMAYE KUSAGA AFUNGUKA KUMILIKI WASAFI TV, WASAFI FM

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amejibu tetesi zinasombaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumiliki vituo viwili vya runinga na radio, Wasafi TV na Wasafi FM.
Akizungumza leo Desemba 4, 2018 katika Kipindi cha Clouds 360, Kusaga alisema; “Ninamiliki Redio zote za vijana kwa namna moja au nyingine. Naamini kwenye ushirika na hivyo kuna biashara nyingi pamoja na Redio nitaendelea kuzianzisha kwa kushirikiana na vijana kwa sababu hilo lilikuwa lengo la Clouds tangu zamani.”
“Utake usitake bila Clouds hakuna Staa yeyote angetokea, hata watukane waseme nini ila bila Clouds wasingekuwa walipokuwa” alisema Kusaga.
Kusaga amesema kuwa anashirikiana na radio nyingine za mikoani kama Safari FM ya Mtwara na Jembe FM ya Mwanza.
Kabla ya kutoa tamko hilo, kulikuwa na maneno kuwa Kusaga ndiye mmiliki wa vituo vya Wasafi TV na Wasafi FM wala si msanii Nasbu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kama wengi wanavyofahamu.

LINNAH Amkana ‘MPENZI’ Wake Mpya KWEUPE!!!

Toa comment