The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Mtolea Achukua Kadi ya CCM

Mwenyekiti wa Wilaya ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, Almishi Hazali (kulia) akimkabidhi kadi ya uanachama ya kujiunga na CCM, aliyekuwa Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea katika Ofisi ya CCM, Kidagaa Kata ya Buza, Temeke.
 ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke, kupitia Chama cha Wananchi, Abdallah Mtolea amechukua kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga rasmi na chama hicho ikiwa ni siku tisa tangu atangaze kujiuzulu uanachama wa CUF, Ubunge na nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama hicho.
Mtolea amechukua kadi hiyo leo Jumamosi, Novemba 24, katika Ofisi za CCM, Kidagaa Kata ya Buza jijini Dar es Saalaam na kukabidhiwa kadi hiyo na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Temeke, Almishi Hazali.
Mtolea ambaye alianza kwa kukabidhi kadi yake ya (CUF) kwa mwenyekiti huyo, amesema ameamua kujiunga na CCM ili aweze kushirikiana kikamilifu na Rais Dkt. John Magufuli katika katika ujenzi wa Taifa.

 

Novemba 15, 2018, Mtolea alijivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya CUF akidai kumekuwa na migogoro mingi ndani ya chama chake. Mtolea alitangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma.

MTOLEA Alivyopokelewa CCM/Ahaidiwa Ubunge Tena

Comments are closed.