The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Nandy Afungukia Kuwa Ujauzito

0

Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Bongo fleva, Faustina Charles Mfinanga, maarufu Nandy amekanusha madai ya kwamba ana ujauzito wa mpenzi wake msanii Billnass.

 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa ubalozi wa moja ya makampuni nchini, mwimbaji huyo aliweka wazi kuwa hatarajii, na kuongeza kuwa atakapopata ujauzito habari hizo hazitafichwa kwa mashabiki wake.

“Kwa sasa hamna ujauzito, na mimi kama unafuatilia swala la ujauzito, huu ni mwaka wa pili sasa ninazungumziwa. Nakumbuka wakati nikifanya nyimbo za Giza Kinene, nimeshiba zangu watu wakasema nina ujauzito. Sasa Ujauzito gani huo ambao haukui, wala sizai?

Watu waache ku-predict vitu, na nikiwa na ujauzito hakuna kitu cha kuficha⁣,” alisema Nandy.

Leave A Reply