The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Pistorious aachiwa huru

oscar-pistorius-800

Oscar Pistorius akiwa mahakamani.

MWANARIADHA mlemavu wa nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp mnamo mwaka 2013.PISTORIOUS (4)

Wazazi wa Reeva Steenkamp wakiwa mahakamani.

Pistorius ameachiliwa huru usiku wa kuamkia leo na kuamliwa kutumikia kifungo cha nje hadi pale atakapomaliza kifungo hicho cha miaka mitano.

Baada ya kuachiliwa huru, alielekea kwa mjomba wake Arnold Pistorius.

PISTORIOUS (5)

Oscar Pistorius akiwa na aliyekuwa mpenzi wake marehemu Reeva Steenkamp.

Mwanariadha huyo alipatikana hatia mwezi Octoba mwaka ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Kama sehemu ya msamaha huo, bingwa huyo wa zamani wa mbio za walemavu atahitajika kukaguliwa kisaikolojia kila baada ya kipindi fulani na hataruhusiwa kumiliki bunduki tena.

PISTORIOUS (3)

…Akisikiliza hukumu.

Familia yake imekanusha madai kuwa ameachiliwa mapema ikisema kuwa japo hayumo gerezani angali anatumikia kifungo chake nyumbani.

Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa hajapunguziwa kifungo na atatumikia kipindi hicho kwa uadilifu kulingana na sheria za taifa.

PISTORIOUS (2)Hata hivyo bingwa huyo wa zamani anakabiliwa na hatari ya kurejeshwa gerezani iwapo kiongozi wa mashtaka atafaulu kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini iliyompata na hatia ya kuua bila kukusudia Steenkamp.

Comments are closed.