Hatimaye Sister Fey Afunga Ndoa na Kiben Ten Chake
MSANII Sister Fey ambae hivi karibuni alikamatwa na kuwekwa rumande kwa amri ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kutokana na kusambaza picha zisizokuwa na maadili wakiwa faragha na mpezni wake Holystar, wawili hao wameamua kufunga ndoa na kuhalalisha mahusiano hayo kimya kimya.
Ikiwa bado watu wanajua kuwa mwanadada huyo yuko rumande, ghafla jana zilianza kusambaa picha zikimuonyesha mwanadada huyo akiwa katika vazi la harusi na mwanaume huyo wakiwa na furaha ya tendo hilo.
Hata hivyo mashabiki na watu mbalimbali wanaamini kuwa kuna kitu kikubwa Sister Fey atakuwa amejifunza baada ya kuwekwa rumande na kukosa wa kumtetea kutokana na ukosefu wake wa maadili na kwa kufunga kwao ndoa basi wataheshimu na kuyachukulia ‘siriazi’ mahusiano yao.
Comments are closed.