Hatimaye Tshisekedi Atangaza Baraza la Mawaziri

RAIS Félix Tshisekedi ametangaza baraza jipya la mawaziri katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya kusubiriwa kufanya hivyo kwa miezi saba.

 

Katika serikali hiyo mpya, wanawake wamepewa asilimia kumi na saba ya mawaziri,  na wanaume asilimia 83.

 

Mnamo Julai mwaka huu Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila, walikubaliana kuunda serikali ya muungano itakayokuwa na mawaziri 66 ambapo chama cha rais huyo wa zamani  kimepata wizara 43, na kile cha  Tshisekedi kimejinyakulia wizara 23.


Loading...

Toa comment