Hausigeli aiba mtoto Dar, akamatwa Mwanza

Na Makongoro Oging’

KAA chonjo! Mfanyakazi wa ndani ‘hausigeli’, Sheila Chacha (pichani) aliyekuwa akifanya kazi kwa Abraham Jullu maeneo ya Tegeta-Wazo, Dar anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Mwanza akidaiwa kuiba mtoto wa tajiri yake aitwaye Coletha (1/8) jijini Dar.

Mfanyakazi wa ndani ‘hausigeli’, Sheila Chacha anayetuhumiwa kwa kuiba mtoto.

Akizungumza na gazeti hili juzi, baba mzazi wa mtoto huyo, alisema mfanyakazi huyo wa ndani alitoweka na mtoto huyo Septemba 22, mwaka huu na haikujulikana alipoelekea.

Baba huyo alisema siku ya tukio, yeye na mkewe walikuwa kazini kama kawaida na kumuacha mfanyakazi huyo na watoto wote, akiwemo Coletha, lakini waliporudi hawakumkuta yeye na mtoto.

Aliendelea kusema kwamba, walipoulizia watoto wengine alipo mfanyakazi huyo, walisema aliondoka na mtoto na hakurudi. Walimsubiri lakini hakurudi hadi kesho yake ndipo wakaenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Wazo Hill Dar na kuandikiwa jalada lenye namba ya kesi WH/8094/2015.

Kwa mujibu wa baba huyo, mfanyakazi huyo alikuwa bado mgeni na mpaka anaondoka alikuwa ametimiza siku 14 tu. Hata hivyo, baba huyo aliongeza kuwa, mfanyakazi huyo alikamatwa maeneo ya Buzuruga jijini Mwanza akiwa na mtoto huyo na kwa sasa anahojiwa ili kujua lengo la kuondoka naye.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!


Loading...

Toa comment