The House of Favourite Newspapers

Hausigeli atoroka, adaiwa kutolewa kafara

0

HII kali! Msichana wa kazi ‘hausigeli’ aliyetambulika kwa jina la Eva Raiton Sindilia (18) anasakwa kwa udi na uvumba na bosi wake, Shomari Mwansopo (35), mkazi wa Mtaa wa Uwanjani wilayani Momba mkoani hapa kufuatia kutoroka nyumbani kwake na kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Mwansopo alisema kufuatia tukio hilo, ndugu wa msichana huyo wanamtuhumu yeye kwamba, ameshiriki mauaji ya binti huyo kwa kumtoa kafara madai yanayompa wakati mgumu bosi huyo.

Mwansopo aliendelea kusema kuwa, kwa mujibu wa majirani, siku ya kutoroka, Eva alikwenda kwa jirani mmoja aitwaye mama Himidini na kuacha funguo kijanja.

“Baada ya kuacha funguo, Eva alitowekea kusikojulikana kitu kilichoniletea matatizo makubwa kwa kupewa kashfa na ndugu zake wakidai kwamba nimemtoa kafara binti yao,” alisema kwa masikitiko Mwansopo.

Alisema sasa ni mwaka mmoja umekatika tangu Eva atoroke Julai 24, mwaka jana ambapo mpaka sasa haijajulikana mahali alipo kutokana na kusakwa kila kona ya ndani ya mkoa mpya wa Songwe na Mbeya bila mafanikio.

Bosi huyo aliendelea kusema kuwa, yeye baada ya kugundua Eva ametoroka  alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Tunduma ili asaidiwe ambapo polisi walimwambia akachukue kibali kwa mwenyekiti wake wa serikali za mtaa ili awe salama.

Alisema kwa upande wake, mwenyekiti wa mtaa huo, Elia Mwahihijo hakuwa na msaada wowote zaidi ya kumpa barua ya kumtafutia binti huyo.

“Kutokana na kushukiwa vibaya na ndugu wa Eva, nawaomba Watanzania wenzangu kwa yeyote atakayebahatika kumuona msichana huyo atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo jirani yake au anipigie simu namba 0754211852, nitamfikiria chochote,” alisema bosi huyo.

Leave A Reply