The House of Favourite Newspapers

Hawa Jamaa ni Noma kwa Mkwanja Afrika Mashariki!

HOTI stori kwenye showbiz ni ripoti ya Jarida la Forbes kwa mwaka 2019.  Forbes wameanika listi ya wasanii matajiri Afrika. Kwenye listi hiyo, staa wa Senegal, Aliaume Damala Badara Thiam ‘Akon’ amewaburuza wenzake, ana utajiri wa shilingi bilioni 183.

 

Kuhusu mambo ya mkwanja kwa wasanii, habari hoti zaidi mpya ni juu ya wasanii wanaoongoza Afrika Mashariki.

Katika wakali hao matajiri, utajiri wao umepatikana kupitia uwekezaji, ubalozi, muziki, majumba na magari;

 

10: RAGGA DEE

Ni mkongwe kutoka Uganda. Dee anapiga muziki aina ya raggae, Hip Hop na Lingala.

Ni staa wa kwanza nchini Uganda kumiliki gari aina ya Hummer. Ukiweka pembeni hilo, mkali huyu amewekeza kwenye majumba na lebo yake ya Buggie Empire.

Dee pia mkwanja wake anatengeneza kupitia matamasha anayoandaa katika nchi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Zambia, Nigeria na Kongo DR.

 

9: BEBE COOL

Bebe ni mkongwe mwingine ambaye aliingia kwenye gemu la muziki wa Reggae mwaka 1997 nchini Kenya na kuhamia Uganda.

Tangu ameingia kwenye gemu na kuachia hits za kutosha, Bebe amekuwa akiingiza mkwanja mrefu uliomuwezesha kumiliki majumba kadhaa ya kupanga maeneo ya Kiwatule, Ntinda na Bukoto huko Uganda.

 

Pia ni Balozi wa Coke Studio Africa na Airtel. Mwaka 2016, aliingiza mamilioni kupitia kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo ambazo alizipata kupitia kwa Rais Museveni.

Bebe anamiliki magari ya kifahari yakiwemo Hummer na Mercedes Benz kadhaa.

 

8: SAUTI SOL

Haina ubishi kwamba Sauti Sol ndilo kundi linalotikisa kwa sasa Afrika Mashariki. Kundi hili lilianzishwa rasmi mwaka 2005.

Sauti Sol wana lebo yao ya Sauti Sol Entertainment ambayo huitumia kurekodi na kuwasimamia wasanii.

 

Mkwanja wao wanautengeneza kupitia Coke Studio Africa, Kampuni ya Kamera ya Niko na Safaricom.

Jamaa hawa ni mabalozi wa vinywaji kama Chrome Vodka, Giants na taasisi mbalimbali ikiwemo British Council.

 

7: ALI KIBA

Kiba ni kati ya wasanii wakubwa Afrika Mashariki akiwa na ushindani mkubwa na Diamond.

Kiba alianza kukubalika mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo tangu aanze muziki ameingiza mkwanja wa kutosha. Inaelezwa kuwa katika kipindi hicho aliwahi kuwa Balozi wa Kampuni ya Tigo, Coke Studio Africa na kampeni ya kupinga ujangili wa Tembo.

Mkali huyu pia aliingiza mkwanja mrefu mwaka 2017 katika kampeni za uchaguzi mkuu Kenya. Kiba anamiliki magari kadhaa ya kifahari ikiwemo BMW X5 na mijengo mbalimbali maeneo ya Tabata, Dar.

 

6: PROFESSOR JAY

Unaweza kumuita Mbunge wa Binadamu na Wanyama kutokana na kuwakilisha Jimbo la Mikumi lililozungukwa na Mbuga ya Wanyama ya Mikumi.

Jay alianza kukubalika kimuziki mwaka 1994 akiwa na Kundi la Hard Blasterz na tangu hapo amepata mafanikio makubwa.

 

Mkongwe huyu ambaye aliingia rasmi kwenye siasa mwaka 2015 na kuwa mbunge, utajiri wake unaelezwa kupatikana kupitia shoo zake tangu aanze muziki na kumiliki studio.

Jay anatembelea magari kadhaa likiwemo Toyota Land Cruiser V8.

 

5: BOBI WINE

Bobi Wine ni kati ya wasanii walioweka alama Uganda.

Ni msanii tajiri namba mbili nyuma ya Jose Chameleone nchini humo ambapo kwa sasa anapiga muziki na ni Mbunge wa Jimbo la Kyaddondo Mashariki baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2016.Anamiliki Ufukwe wa One uliopo Lake Victoria, shamba kubwa katika Kijiji cha Gomba akiwa na mifugo kibao.

 

Ana lebo yake ya Firebase Records. Pia ana jengo kubwa la biashara la Ssemakokiro Plaza na majumba ya kifahari huko Magere na Gomba.

Bobi ana boti mbili, moja ikiwa na sifa ya kuwa na spidi ya hatari huku pia akiwa amewekeza kwenye biashara ya teksi.

Bobi ni balozi wa Benki ya Centenary, Mtandao wa Simu wa MTN, mipira ya kiume ya Life Guard na ni mshauri katika Wizara ya Afya.

 

4: AKOTHEE

Ukimuona anajichetua mitandaoni huwezi kumdhania kama msanii Akothee wa Kenya ni miongoni mwa wasanii wenye utajiri Afrika Mashariki.

Katika 10 bora, Akothee ni msanii pekee wa kike anayetikisa kwa utajiri. Mwanamama huyu anayependa kujiita Madam Boss amewekeza kwenye muziki na majumba makubwa ya kukodi anayoyaita Akothee Properties.

Anamiliki kampuni ya utalii ya Akothee Safaris na fukwe ya kifahari ya Morning Star Dian iliyopo Dian, Kenya.

 

Kama ilivyo kwa Bobi, Akothee amejiingiza kwenye biashara ya teksi mjini Mombasa. Katika mahojiano anakiri kumiliki mjengo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2 uliopo Rongo, Migori. Jumba lingine la kifahari ndani ya Fukwe za North- Coast lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.6 na lingine katikati ya Nairobi lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7.

Mwanamama huyu hadi Zurich nchini Switzerland anamiliki mjengo wa vyumba vinne vya kulala.

Anamiliki magari ya kifahari kama Mercedes AMG SL63 Convertible Roadster, Audi Limousine, Range Rover na Toyota Land Cruiser V8.

 

3: JAGUAR

Kama ilivyo kwa Jay na Bobi, Jaguar alianza muziki mwaka 2005 na sasa ni mbunge akiwa anawakilisha Jimbo la Starehe, Kenya.

Hitmaker huyu wa Ngoma ya Kigeugeu, utajiri wake kwa kiasi kikubwa unatokana na biashara ya usafiri (kuingiza na kuuza magari), ujenzi wa majengo, vyombo vya moto (pikipiki, Bajaj na magari), ujenzi wa majengo ya kukodi na muziki.

 

Utajiri mwingine ameupata kupitia lebo yake ya MainSwitch Productions. Anamiliki mijengo pande za Athi-River, Nairobi na mmoja uliopo kijijini Nyeri.

Jaguar anamiliki Range Rover, BMW kadhaa, Toyota Land Cruiser, Bently, Jaguar na Mercedes Benz-E-Class.

Pia jamaa ni balozi wa Coke Studio Africa na mmoja wa viongozi katika kampeni ya kupinga madawa ya kulevya.

 

2: DIAMOND

Unaweza kumuita Mondi au Chibu Dangote! Ni staa wa Bongo Fleva akiwa amenza safari yake ya muziki kutoka uswahilini; Tandale, Dar.

Tangu aingie kwenye gemu, amekuwa akiingiza pesa nyingi kupitia shoo za ndani na nje ya nchi. Utajiri wake unatajwa kupatikana kupitia shoo zake, ubalozi na kumiliki Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo inawasimamia wasanii kama Queen Darleen, Rayvanny, Mbosso na Lava Lava.

Utajiri mwingine amepata kupitia TV (Wasafi TV), redio (Wasafi FM), studio ya video (Zoom Production) na studio ya muziki (Wasafi Records).

 

Mondi ni balozi wa sabuni (Niceone), vinywaji kama Pepsi na Luc Belaire, michezo ya kubashiri (Parimatch), aliwahi kuwa Balozi wa Vodacom, Fenicha za majumbani (Danube), usafiri (Uber), viungo vya vyakula (Red Gold), Karanga (Diamond Karanga), Coke Studio Africa, Chaneli ya TV (Dstv) na pafyumu (Chibu).

Anamiliki nyumba moja Madale, Dar na nyingine Afrika Kusini. Upande wa magari ya kifahari ana Toyota Land Cruiser V8 na BMW X6 achana na yale aliyomzawadia mama mpenzi wake.

 

1: JOSE CHAMELEONE

Ni lejendi wa muziki Afrika Mashariki akiwa na zaidi ya miaka 20 kwenye gemu akiwakilisha Uganda.

Utajiri wake unaelezwa kutokana na Fukwe za Coco zilizopo Ziwa Victoria, majengo ya kukodi anayoyaita Daniella Villas yaliopo Bweyogerere, lebo ya muziki ya Leone Island na nyumba nyingine za kukodi zilizopo Barabara ya Entebbe, Uganda.

 

Ni msanii anayelipwa pesa nyingi Afrika Mashariki akiwa anashikilia rekodi ya kujaza watu wengi katika tamasha moja lililofanyika nchini humo mwaka 2014 lililohudhuriwa na mashabiki 40,000.

Ameingiza mamilioni kupitia shoo alizofanya Uingereza, Marekani, Ujerumani, Sweden, Ubelgiji, Malaysia, China na Afrika Kusini.

 

Ni balozi wa mtandao wa simu wa MTN, Simu za Idroid, Coke Studio Africa, kampuni ya utalii ya Busoga, Startimes Uganda, Pepsi na nyingine nyingi.

Anamiliki pia majumba mawili ya kifahari katika Milima ya Seguku nje ya Entebbe yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 740 na jumba lingine analo Muyenga, Kampala lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 959.

 

Majengo yake mengine ya kifahari yapo Arizona, Marekani na Kigali, Rwanda.

Upande wa magari anamiliki Bently Continental GTC Convertible, Cadillac Escalade SUV, Hummer, 2017 Dodge Charger, Range Rovers, Land Rover LR4, Ford, BMW X5, 1973 Mercedes classic, Toyota Land Cruiser VX, BMW Convertible na Mercedes Benz ML270.

ANDREW CARLOS

 

Comments are closed.