The House of Favourite Newspapers

HAWA NDO WATU 10 WENYE NGUVU YA USHAWISHI ZAIDI DUNIANI 2018

KUWA mmoja kati ya watu wenye nguvu kubwa duniani sio jambo rahsisi,inakupasa uwe na ushawishi mkubwa sana kwa hao hao watu na leo utawajua watu 10 ambao wana nguvu na uwezo mkubwa sana kwenye fedha, ushawishi na wamesimamisha majina yao katika uongozi na biashara duniani.

 

Takwimu hii ni ya mwaka 2018 na imetolewa na Jarida maarufu la Biashara, ‘Forbes’

 

  1. Mmiliki Wa Google – Larry Page (45)

Larry Page alizaliwa 1973  Califonia na ana elimu ya Kompyuta Sayansi, ni Mjasiriamali wa masuala ya mitandao anayemiliki mtandao wa Google. Utajiri wake ni kiasi cha Dola Billion 38.8.

 

09. Waziri Mkuu wa India – Narendra Modi (68)

Narendra Modi alizaliwa 1950 Gujarat India, amekuwa katika nafasi ya Waziri mkuu tangu mwaka 2014. Kwa mwaka mmoja wa kwanza wa Waziri huyo pato la taifa la India Lilipanda mpaka kufikia Asilimia 7.4.

 

Kwa muda wa miaka miwili, kiongozi huyo anaonekana akifanya vizuri sana baada ya kuboresha hali ya afya pamoja na usafi wa mazingira kwa kiwango cha juu, pia ametengeneza mahusiano mazuri kati ya taifa lake na mataifa mengine.

 

08. Mtoto Wa Mfalme Salman – Mohammed bin Salman Al Saud (33)

Amezaliwa mwaka 1985 Riyadhi huko Soud Arabia na ni mkurugenzi wa Baraza la Uchumi na Maendeleo, pia ni mkurugenzi wa Baraza la Siasa, Mambo ya Usalama na Waziri wa Ulinzi.

 

07. Mmiliki Wa Microsoft – Bill Gates (63)

Alizaliwa mwaka 1955 Seattle huko Washington Marekani.

Ni mfanyabiashara, mwekezaji na mtaalam wa program za kopmyuta ambaye amesoma Chuo Kikuu cha Harvard. Mwaka 1975 walianzisha Kampuni ya Microsoft akiwa na mwenzake Paul Allen. Microsoft Os ni programu yenye nguvu sana duniani kwa kompyuta.

 

Bill Gates amekuwa akitajwa na Forbes kuanzia mwaka 1987. Anashikilia nafasi ya kwanza kwa utajiri wa Dunia akijikusanyia mkwanja wa Dola Billioni 78.3.

 

06. Papa w Kanisa Katoliki – Jorge Mario Bergoglio (Pope Francis) (81)

Alizaliwa mwaka 1936 huko  Argentina, ni kiongozi wa dini ya Wakristo (RC) duniani kote. Alikalia kiti cha upapa tangu mwaka 2013 akichukua nafasi ya Papa Benedicto wa XVI ambapo ameshikilia nafasi ya 266 na ni wa kwanza kutoka Bara la Amerika.

 

05. Mmiliki wa Amazon – Jeff Bezos (54)

Alizaliwa 1964 New Mexico huko Marekani. Ni  mfanyabiashara, mjasiriamali, mwekezaji na anajihusisha na mwasuala ya teknolojia. Amazon ni Kampuni kubwa sana ya kibiashara ya mtandaoni ambayo makao yake makubwa ni  Washington.

Amazone.com inajihusisha na kuuza bidhaa mtandaoni kama, vitabu, kuuza na kusikiliza nyimbo (Audio & video), Softiware, Video games, nguo, Chakula, Toys, vitu vya samani na bidhaa nyingine nyingi. Anamiliki utajiri wa Dola Billion 125.8

 

04. Waziri Mkuu wa Ujerumani – Angela Markel (64)

Alizaliwa mwaka 1954 Hamburg huko Magharibi mwa Ujerumani. Amekuwa Councilor  wa Ujerumani tangu mwaka 2005 mpaka wakati huu bado anaishikilia nafasi hiyo.

 

03: Raisi wa Marekani – Donald Trump (72)

Alizaliwa mwaka 1946 huko New York. Ni rahisi wa 45 wa Marekani na ametoka kwenye familia tajiri yenye uwezo wa kifedha.

Donald Trump ndiyo rahisi wa kwanza wa marekani Tajiri kuliko maraisi wengine waliotangulia. Anamiliki utajiri wa kiasi cha Dola za Marekani Billion 3.1 tofauti na mwaka jana ambapo alikuwa akimiliki Dola Billion 3.9.

 

02. Rais wa Rassia – Vladmar Putin (66)

Alizaliwa mwaka 1952 Saint Petersburg huko Russia.

Ni raisi wa Russia tangu mwaka 2012. Kabla hajakalia Kiti cha Urais alikuwa Waziri Mkuu kwa mwaka 1999 na 2000, baadaaye akashika wadhifa huo mwaka 2008 hadi 2012.

 

01: Rais wa China – Xi Jinping (65)

Alizaliwa mwaka 1953 Beijing huko China. Ni Raisi wa China na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China, ni Mkurugenzi wa Tume ya Kuu ya Kijeshi, pia ni Kiongozi wa Tume ya Mageuzi ya Kijeshi na Mtandao.

MTOLEA Alivyopokelewa CCM/Ahaidiwa Ubunge Tena

Comments are closed.