Hawa Ndo Watu Watano wa Ajabu Zaidi Kuwahi Kutokea Duniani – Picha

Unaweza kufikiri umewahi kuona vitu vya ajabu, vingine vikiwa katika picha zilizotengenezwa makusudi kwa kompyuta.  Lakini picha zifuatazo zilipigwa kabla ya ujanja wa kutumia kompyuta kwa njia ya ‘photoshop’ kuzifanyia kila ‘mchezo’ ili zionekane ya ajabu.  Picha zifuatazo zilipigwa kabla ya ujanja huo wa kompyuta, hivyo unabidi kuziona ili uamini.  Ni za kweli.

1. Ella Harper, “The Camel Girl”

Ella  aliyejulikana kama “Twiga Msichana” (Camel Girl), aliishi kuanzia mnamo mwaka 1870 hadi 1921, akiwa amezaliwa huko Handersonville, Tennessee, Marekani, na hali isiyo ya kawaida ya mifupa yake ya miguu ambapo ilikuwa imepinda mithili ya mnyama na hivyo kumfanya aonekane kioja.  Na ndiyo maana ya kuitwa “Twiga Msichana”!.

2. Fannie Mills, “The Ohio Big Foot Girl”

Fannie alizaliwa na hali ya ugonjwa uitwao  Milroy Disease ambayo iliifanya miguu yake kuongezeka umbo na kuwa mikubwa sana.  Alijulikana kama “Msichana wa Miguu Mikubwa wa Ohio” (The Ohio Big Foot Girl).  Alizaliwa hiko Sussex, England, na aliweza kuolewa kabla ya kufariki mwaka 1899, wakati miguu yake ilikuwa imeongezeka ukubwa na kufikia nchi 17 (sentimita 43.18).

3. Maurice Tillet, “The French Angel”

Huyu alikuwa ni mcheza mieleka wa Ufaransa aliyezaliwa Russia.  Alijulikana kama “Malaika wa Ufaransa” (The French Angel). Yeye alikuwa na tatizo linalojulikana kama acromegaly, ambalo ni tatizo la homoni za mwili kuwa na dosari ya kukua kuliko kawaida, hivyo kumfanya mtu awe na viungo vikubwa zaidi ya kawaida vya mwili wake wote.

4. Francesco A. Lentini

Frank alijulikana sehemu kubwa duniani kwa kuwa na mguu wa tatu ambao ulikuwa unafanya kazi kama kawaida.  Mguu huo ulitoana na mchakato kuwepo pacha wake, mchakato ambao haukukamilika tumboni mwa mama yake.

5. Jean Libbera, “The Double-Bodied Man”

Jean alijulikana kama “Mtu Mwenye Miili Miwili” (The Double-Bodied Man).  Alizaliwa jijini Rome, Italia, naye alikuwa na hali kama iliyompata Frankie; yaani kuwa na sehemu ya mwili wa mtu ambaye alikuwa awe pacha wake. Sehemu ya mabaki ya pacha wake ambaye alikuwa azaliwa naye, yalibakia na kuendelea kuwa katika sehemu ya kifua chake hadi kifo chake  Hivyo ndivyo, Jean alivyokuwa — tangu kuzaliwa mpaka akaoa na kupata watoto wanne.

 

Toa comment